WEKUNDU wa
Msimbazi Simba na Chama la wana Stand United kesho wanatarajiwa kuendeleza ubabe katika viwanja viwili tofauti, kusaka pointi
tatu zitakazowapa nafasi ya kuendelea kuongoza katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba itakuwa Uwanja
wa Uhuru ikiikaribisha Kagera Sugar huku
Stand United ikiwa ni mwenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Hizi ndizo timu zinazokimbizana kwa pointi hivyo, macho yote yataelekea kwao.
Simba ndio
vinara wa ligi kwa pointi 20 katika michezo nane waliyocheza, wakijivunia kutopoteza
mchezo tangu kuanza kwa ligi msimu huu.
Timu hiyo ya
Msimbazi huenda ikaendeleza ushindi baada ya kutoka kuifunga Mbeya City mabao
2-0 ugenini, kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya Jumatano.
Lakini pia,
Kagera Sugar haiko katika kiwango kibaya msimu huu, kwani inashika nafasi ya
tatu ikiwa na pointi 15 katika michezo tisa iliyocheza.
Kocha wa Kagera
Sugar, Mecky Mexime alisema anataka kuvuruga sherehe za Simba kwa kuhakikisha
wanainyamazisha.
Licha ya tambo
za wenyeji, itakumbukwa msimu uliopita Simba ikiwa katika kiwango kibaya
iliifunga Kagera Sugar, ambayo nayo ilikuwa kiwango kibaya bao 1-0.
Mchezo huo
huenda ukawa mgumu, kwani Simba itataka kushinda ili kuendelea kubaki kileleni,
na Kagera inataka ushindi iendelee kuwa katika nafasi nzuri katika msimamo wa
ligi hiyo yenye jumla ya timu 16.
Aidha, kama
ilivyo kwa Simba hata Stand United imekuwa ni bora ikijivunia kutopoteza mchezo
hata mmoja. Leo itaikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa CCM, Kambarage
Shinyanga.
Timu hiyo msimu
huu imekuja kivingine baada ya kuwapiga vigogo wawili kwenye uwanja huo, yaani
Yanga na Azam zote zikifungwa bao 1-0 kila moja.
Hio ndio timu
inayoifukuzia Simba kwa pointi 19 hivyo, ni lazima itapambana kuendelea kulinda
nafasi yake. Inakutana na timu ambayo ambayo iko katika kiwango cha kawaida
ikiwa na pointi tisa katika michezo tisa.
Pia, Mtibwa
Sugar inayoshika nafasi ya tano kwa pointi 14 nayo itaendelea kusaka ushindi
kwenye Uwanja wa Manungu dhidi ya
Tanzania Prisons ambayo nayo, haiko vizuri sana msimu huu, ukilinganisha na
msimu uliopita.
Tanzania Prisons
inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 10 katika michezo nane iliyocheza. Timu zote mbili zinahitaji ushindi kwani atakayepoteza atakuwa kwenye uwezekano wa
kushuka kutoka nafasi moja hadi nyingine.
JKT Ruvu na
Mwadui zitakutana zote zikiwa haziko katika nafasi nzuri. Mwadui ina pointi
nane katika michezo nane ikishika nafasi ya tatu kutoka mwisho, na JKT Ruvu
inashika nafasi ya nne kutoka mwisho ikiwa na point inane sawa na Mwadui.
Kila mmoja
anahitaji ushindi kujiondoa katika hatari ya kushuka daraja. Vile vile,
Majimaji ambayo inashika mkia itakuwa ugenini dhidi ya Toto African kwenye
uwanja wa CCM, Kirumba, Mwanza.
Timu hiyo ina
pointi tatu ikishika nafasi ya mwisho, ikifuatiwa na Toto inayoshika nafasi ya
pili kutoka mwisho ikiwa na point inane, wote wakiwa wamecheza michezo tisa.
No comments:
Post a Comment