TIMU ya
Mieleka ya Ngome, imetwaa kombe la mashindano ya mieleka ya kumuenzi baba wa
Taifa, Hayati Julius Nyerere yaliyokuwa yanafanyika kwenye Uwanja wa Ndani wa
Taifa.
Ngome
imeibuka bingwa baada ya kupata medali za dhahabu tatu, fedha mbili na shaba
tatu ikifuatiwa na JKT ambayo ilipata medali za dhahabu mbili, fedha tatu na
shaba nne.
Nafasi ya
tatu ilichukuliwa na magereza ambao walitawala kwenye uzito wa juu ikiwa na
medali za dhahabu mbili, fedha mbili na shaba moja.
Mashindano
hayo ambayo yalishirikisha timu tano, yalishuhudia timu za WWC na Tanga Stars
zikiondoka bila medali.
Akizungumza
baada ya kukabidhi kombe kwa washindi, Mwenyekiti wa Chama cha Mieleka (AWATA)
Andrew Kapelela alisema wameandaa mashindano hhayo ili kumuenzi baba wa Taifa,
Julius Nyerere kwa vile alikuwa anapenda michezo.
"Sisi
AWATA tumemuenzi baba wa Taifa kwa kucheza mchezo wetu na naamini kila chama na
taasisi watamuenzi kwa kufanya kile kilichopo kwenye chama chao", alisema
Kapelela.
Mashindano
ya mieleka yalianza Octoba 10 na kuhitimishwa Octoba 13 na hufanyika kila mwaka
kumuenzi baba wa Taifa, Julius Nyerere.
No comments:
Post a Comment