Akizungumza
na wandishi wa habari jana, Manji alisema wanachama wa klabu ya Yanga
wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo ambao Makao makuu ya klabu
Jangwani, Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili masuala mbali mbali likiwemo
suala la ukodishwaji wa timu ya Yanga.
"Mkutano utakuwa huru na wa haki kwa kila mwanachama ambaye amelipia kadi yake atapewa nafasi ya kutoa maoni na dukuduku lake kabla ya makubaliano kufikiwa," alisema Manji.
"Mkutano utakuwa huru na wa haki kwa kila mwanachama ambaye amelipia kadi yake atapewa nafasi ya kutoa maoni na dukuduku lake kabla ya makubaliano kufikiwa," alisema Manji.
Pia Manji
alisema amesikia kwenye vyombo vya habari (siyo gazeti hili) kuwa Katibu wa
baraza la wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali kuwa hajalipa ada ya uanachama
jambo ambalo linamwondolea sifa ya kuwa mwanachama lakini Akilimali
amelithibitishia gazeti hili kuwa yeye ni mwanachama hai kwani kadi yake
amelipia mwaka mzima.
Manji
alisema baada ya makubaliano hayo ya mkutano mkuu huo kufanyika uwanja wa
mazoezi utaanza kujengwa ndani ya siku 90 katika eneo la Gezaulole lililopo
Kigamboni kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa na kampuni ya Yanga.
Aidha Manji alisema kuhusu suala la kusainiwa kwa mkataba na bodi ya wadhamini dhidi ya kampuni ya Yanga Yetu kila kitu kitajadiliwa kwenye mkutano huo ambapo wanachama wametakiwa kuwahi mapema huku ulinzi ukiwa ni uhakika.

“Kama
itaonekana kuna mgongano wa kimaslahi baina yangu na Yanga kwani Yanga yetu
ambayo inakodishiwa timu mimi ndio mmiliki na Yanga napo mimi ndio Mwenyekiti
basi wanachama wataamua kama naweza kuendelea au nijiuzulu”, alisema Manji
Manji
alisema badala ya wanachama kukimbilia kwenye vyombo vya habari kuongea kuhusu
masuala ya klabu wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo ili
kuchangia kwa manufaa ya Yanga.
Mkutano huu
wa dharura unafanyika huku kikuwepo sitonfahamu ya namna mkataba wa ukodishwaji
wa klabu ya Yanga kwa kampuni ya Yanga yetu ulivyosainiwa kabla ya kuridhiwa na
kamati ya utendaji na baadaye mkutano mkuu.
No comments:
Post a Comment