Mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi. Wa kwanza kulia waliokaa ni mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo, wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.
Mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo kiongeana waandishi wa wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi wa Sprite BBall Kitaa. Wa kwanza kushoto waliokaa ni mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani na wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.
*************************
Miamba
miwili ya mpira wa kikapu kutoka nchini Malawi imewasili jijini Dar es
Salaam leo kwa ajili ya mfululizo wa mechi za kirafiki za kimataifa
dhidi ya timu za bigwigs Jogoo, East Zone One, Mbezi na West Zone Three.
Mechi hizo zenye hamasa ya aina yake zitachezwa kwenye uwanja Bball
Kitaa Park, karibu na Ukumbi wa Gymkhana.
Kulingana
na ratiba iliyotolewa na mratibu wa Bball Kitaa Karabani Karabani pazia
la michezo hiyo litafunguliwa kesho ambapo East Zone One watakipiga na
Bricks, mchezo unaotabiriwa kuwa ni mgumu na wa kusisimua. Siku hiyo
hiyo Mbezi watacheza na Associate Team, mchezo ambao pia unatazamiwa
kuwa na ushindani mkubwa.
Michezo
hiyo bado itaendelea kuwateka wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ambapo
West Zone Three watapambana na Bricks kabla ya Jogoo kuwakaribisha
Associate team. “Tuna furaha kubwa kuandaa michezo hii ya kirafiki. Ni
moja ya sehemu muhimu katika kudumisha mahusiano, vile vile kuendeleza
vipaji vinavyochipukia”, Karabani alisema.
Ujio
wa Bricks na Associate teams jijini Dar es Salaam imeonekana si jambo
geni baada ya timu za East Zone One na West Zone Three kwenda Malawi
mwaka jana. Zikiwa nchini humo, timu hizo zilishinda mechi zao kadhaa.
Karabani
ambaye michuano yake ya mpira wa kikapu iko chini ya udhamini wa
Sprite, amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuibua na kukuza vipaji vya
vijana kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo michuano hiyo imekuwa
ikifanyika. Vilevile michuano hii inatoa fursa ya kuendeleza ushirikiano
baina ya maeneo mbalimbali ya ndani ya nje ya nchi.
“Lengo
letu ni kuanzisha michuano ngazi ya kanda mwishoni mwa mwaka huu,
ambapo mabingwa kutoka Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe”, Karabani
alisema na kuongeza kuwa uzinduzi wa michuano hiyo utafanyika nchini
Malawi
Kwa
upande wake, Meneja Biashara wa Coca-Cola nchini, Maurice Njowoka
alisema anajisikia furaha kubwa kutokana na heshima waliopewa kuisapoti
michuano hiyo hapa nchini na kusisitiza kuwa kampuni yake itaendeleza
ushirikiano wake na wadau wa mchezo wa kikapu kuzidi kuutangaza mchezo
huo.
“Sote
tunafahamu kuwa mpira wa kikapu ni moja ya michezo maarufu na yenye
nguvu nchini, hasa miongoni mwa vijana ambao wanahitaji aina hii ya
msaada ili kuhamasika na kuweza kuendeleza vipaji vyao”, Njowoka
alisema.
No comments:
Post a Comment