Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA limekubali kutumia teknolojia ya kudhibitisha goli kama mpira umeingia golini maarufu goal-line katika mashindano ya Euro 2016 yanayotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa.
Makubaliano
hayo yamefikiwa katika kikao cha kamati ya utendaji ya UEFA iliyokutana
katika makao makuu ya UEFA yaliyopo Nyon, Switzerland wakati kamati
hiyo ilipokutana kwa ajili ya kujadili mambo ya msingi kwa ajili ya
mashindano ya mwaka huu ya Euro ambayo yanatarjiwa kuanza mwezi Juni
mwaka huu.
Pamoja
na kuanza kutumia teknolojia hiyo katika mashindano ya Euro 2016 pia
kamati hiyo ya utendaji imekubaliana kuanza kutumia teknolojia hiyo
katika mashindano ya ligi ya Mabingwa Ulaya kuanzia msimu ujao wa
2016/2017.
No comments:
Post a Comment