Kikosi cha Real Madrid.
Real
Madrid ya Hispani imefanikiwa kuongoza katika listi ya klabu tajiri
duniani katika orodha iliyotolewa na kampuni ya Deloitte ambayo
inajihusisha na kufatilia matumizi na ukusanyaji wa fedha kwenye vilabu.
Katika
orodha imeyotolewa na kampuni hiyo imeitaja Real Madrid kama klabu
tajiri duniani ikiwa na utajiri unaokadiliwa kufikia Pauni Milioni 439
kwa mwaka 2014/2015 na ikifuatiwa na washindi wa kombe la ligi ya
mabingwa Ulaya, Barcelona ambayo inautajiri wa Pauni Milioni 427.
Nafasi
ya tatu inakamatiliwa na Manchester United ambayo imeshuka kwa nafasi
moja kutoka nafasi ya 2 na sasa inashika nafasi ya tatu ikiwa na utajiri
unaokadiliwa kufikia Pauni Milioni 365.2.
No comments:
Post a Comment