Kiungo
wa Chelsea na timu ya taifa ya Brazil, Ramires anatarajiwa
kusajiliwa na klabu ya Jiangsu Suning usajili unaotarajiwa
kukamilika muda wowote kuanzia sasa.
Ramires,
28 anatarajiwa kuondoka Chelsea ambayo alijiunga
mwaka 2010 akitokea Benfica ya Ureno kwa ada ya Pauni Milioni 17 na
anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo ya China kwa ada ya Pauni Milioni 25.
Oktoba
mwaka jana Ramires alisaini mkataba na Chelsea wa miaka minne na sasa
wana muuza Jiangsu ambayo inaongozwa na mchezaji wa zamani
wa Chelsea, Dan Petrescu na kwa msimu wa 2015 ilimaliza katika nafasi ya
tisa na kufanikiwa kushinda kombe la China (Chinese Cup 2015).
Akiwa
na Chelsea, Ramires alifanikiwa kushinda kombe la Ligi Kuu ya
Uingereza, Kombe la FA, Capital One, kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya na
Kombe la Ligi ya Europe yote mara moja moja.
No comments:
Post a Comment