MENEJA
wa Manchester United Louis van Gaal Leo amesafiri kwenda Germany na
Wachezaji 19 kwa ajili ya Mechi yao ya mwisho ya Kundi B la UEFA
CHAMPIONS LIGI, UCL, ambayo itaamua kama watasonga Raundi ya Mtoano au
watatupwa EUROPA LIGI.
Man
United hawawezi kutupwa nje kabisa ya Ulaya kwani matokeo ya aina
yeyote ama yatwabakisha UCL au kupelekwa EUROPA LIGI wakimaliza katika
Nafasi ya 3 ya Kundi B.
Katika
Kikosi hicho cha Wachezaji 19 hayupo Kepteni Wayne Rooney na Kiungo
Morgan Schneiderlin ambao ni Majeruhi na wanaungana na Majeruhi wengine
Marcos Rojo, Ander Herrera, Phil Jones, Luke Shaw na Antonio Valencia.
UEFA CHAMPIONS LIGI
KUNDI: B:
PSV Eindhoven (Pointi 7) v CSKA Moskva (4)
Wolfsburg (9) v Manchester United (8)
-Wolfsburg watafuzu wakipata Sare na watachukua Nafasi ya Kwanza wakishinda.
-Man United watasonga wakishinda na kuwa Washindi wa Kundi.
-PSV watafuzu wakishinda au wakidroo ikiwa Man United itafungwa
-CSKA watatwaa Nafasi ya 3 wakiifunga PSV.
Miongoni
mwa Kikosi hicho wapo Chipukizi kadhaa akiwemo Paddy McNair ambae
alitolewa Haftaimu kwenye Droo na West Ham Majuzi na nafasi yake
kuchukuliwa na Chipukizi wa Uruguay Guillermo Varela ambae nae yupo
safarini.
Chipukizi wengine Kikosini ni Nick Powell, ambae muda
mrefu hajajumuika katika Kikosi cha Kwanza na pia wapo Kiungo Sean Goss
na Beki Cameron Borthwick-Jackson.
Kikosi kamili:
David De Gea, Sergio Romero; Paddy McNair, Chris Smalling, Guillermo
Varela, Cameron Borthwick-Jackson, Daley Blind, Matteo Darmian; Bastian
Schweinsteiger, Michael Carrick, Sean Goss, Nick Powell, Ashley Young,
Jesse Lingard, Andreas Pereira, Juan Mata; Memphis Depay, Marouane
Fellaini, Anthony Martial.

Memphis Depay kwenye mazoezi huko Volkswagen Arena akijiweka tayari kupambana leo hii usku kwenye hatua ya mwisho

Van Gaal akiwacheki Vijana wake kwenye mazoezi kujiweka sawa dhidi ya Wolfsburg

No comments:
Post a Comment