Manchester
United imefungwa 3-2 na Wolfsburg Bao 3-2 kwenye Mechi ya Kundi B la
UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL na kutupwa nje na sasa kucheza Raundi ya Mtoano
ya EUROPA LIGI.
3-2
Kipigo
hicho, na ushindi wa PSV Eindhoven wa Bao 2-1 dhidi ya CSKA Moscow,
kumezifanya Wolfsburg na PSV kufuzu kwenda Raundi ya Mtoano ya UCL na
Man united kumaliza Nafasi ya 3.
Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Wolfsburg kucheza Raundi ya Mtoano ya UCL. 
Naldo akipeta...
Huko
Santiago Bernabeu, Cristiano Ronaldo alifunga Bao 4, Karim Benzema
kupiga 3 na moja la Mateo Kovacic na kuwapa ushindi Real wa Bao 8-0 toka
Kundi A.
Real, na PSG, ambao wameshinda 2-0 walipocheza na Shakhtar Donetsk zote zimesonga na Shakhtar itakwenda EUROPA LIGI.
Man
City, ambao walikuwa washafuzu toka Kundi D, Leo wameichapa Borussia
Mönchengladbach 4-2 na kumaliza kileleni mwa Kundi hilo na kufuatiwa na
Juventus ambao Leo walifungwa 1-0 na Sevilla ambao wamemaliza Nafasi ya 3
na hivyo kwenda EUROPA LIGI.
Van Gaal akipagawa baada ya kutupwa nje

Naldo ndiye aliyepeleka kilio baada ya kufunga bao la tatu kwa Wolfsburg

Naldo akitupia kwa kichwa mpira wa kona

Akitupia bao la pili

Mata akishangilia bao

Man United wakipongezana...

Akishangilia bao

1-1

Raha ya kufunga bao!

Kikosi cha Man United

Van Gaal

Sir Alex Ferguson

Sir Bobby
No comments:
Post a Comment