Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 14, 2015

ARSENE WENGER ATAKIWA NA (FA) KUFAFANUA MADAI WACHEZAJI KUTUMIA MADAWA MARUFUKU

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger, ametakiwa na FA, Chama cha Soka England, kutoa ufafanuzi wa madai yake ya matumizi ya Madawa marufuku kwa Wachezaji.
Akihojiwa na Jarida la huko France, L'Equipe, Wenger anadaiwa kutamka ‘sijamdunga Mchezaji wangu ili awe bora lakini zipo Timu alizopambana nazo hazikuwa na fikra hizo.’
Mwezi Septemba kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI, Arsenal ilipigwa 2-1 na Dinamo Zagreb na Mchezaji wa Timu hiyo, Arijan Ademi, kugundulika anatumia Madawa marufuku.
Hivi sasa uchunguzi kuhusu Kesi ya Ademi unaendelea na vinangojewa vipimo vya pili vyake ili kuthibitisha utumiaji huo wa Madawa marufuku na endapo itathibitika ni wazi Mchezaji huyo atafungiwa.

FA imetoa Taarifa yao kwamba wao, wakishirikiana na Mamlaka ya Kuzuia Matumizi ya Madawa Marufuku ya Uingereza, Ukad [United Kingdom Anti-Doping], wana uchunguzi wa kina kupima wakiukaji wa matumizi ya Madawa hayo na ni mara chache mno Wachezaji wao wamebambwa kwa kosa hilo na ikitokea hilo basi kila kitu huanikwa hadharani.

No comments:

Post a Comment