Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 28, 2015

ARSENAL YAPIGWA FAINI NA KUONYWA

Klabu ya Arsenal imepigwa Faini Pauni 60,000 na kuonywa baada ya kukiuka Kanuni za Mawakala wa Soka kwenye Uhamisho wa Mchezaji Calum Chambers.
FA, Chama cha Soka England, kimeipata Arsenal na hatia ya kumtumia Wakala asie rasmi na asiekuwa na Leseni ‘kumrubuni’ Mchezaji huyo.
Ingawa Arsenal imejitetea haikufanya kosa lakini wao pamoja na Wakala Alan Middleton wamepatikana na hatia na Wakala huyo kupigwa Faini ya Pauni 30,000 na kusimamishwa kwa Miezi Mitatu. 

Beki Calum Chambers alijiunga na Arsenal Julai 2014 kutoka Southampton kwa Dau la Pauni Milioni 16.
Taarifa ya FA imesema Arsenal ilikiri baadhi ya makosa yao na kukana mengine huku wakijitetea hawakuwa wanajua kwamba Wakala wa Mchezaji huyo hakuwa na kibali cha kufanya kazi hiyo hivyo kutoruhusiwa kuendesha Uhamisho wa Mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment