KAULI ya
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, kuwa ameacha kwenda kutazama mechi za timu ya
Taifa kutokana na watu kudai akija timu hiyo ndipo inapofanya vibaya imemfanya
kocha Mkuu wa Timu ya Taifa, Charles Boniface Mkwasa kumwomba aweke silaha chini na kuisapoti
Akizungumza
na wandishi wa habari jana Mkwasa alisema anamwomba Kikwete aweke silaha chini
na kuanza kwenda uwanjani kwani uwepo wake utawapa morali wachezaji
“Wachezaji
wetu walikuwa hawajui maana ya uzalendo sasa wanaelewa baada ya kuwafundisha
hivyo uwepo wa Rais Kikwete utawafanya waonyeshe uzalendo kwa kucheza kwa nguvu
zao zote hivyo namwomba aachane na kauli hiyo tugange yajayo”, alisema Mkwasa.
Wakati
akifunga bunge mjini Dodoma, Rais Kikwete alitoa hotuba yake kwa wabunge na
kuelezea jinsi ambavyo amesaidia michezo ikiwemo soka kwa kuwaleta makocha
mbalimbali lakini timu hiyo imekuwa ikiendelea kufanya vibaya jambo
lililomfanya kuacha kwenda kuitazama wakati ikicheza.
No comments:
Post a Comment