Mkufunzi wa FIFA Elaxander kutoka Ufaransa (aliye katikati ya waliosimama) kwa pamoja na washiriki wa kozi ya makocha wa golikipa inayoendelea katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam |
MAKAMU Mwenyekiti
wa Bodi ya Ligi nchini, Said Mohamed amewataka washiriki wa kozi ya makipa
kutumia vizuri mafunzo watakayopata katika kuendeleza mpira nchini.
Said Mohamed
ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya TFF, aliyasema hayo jana wakati
akifungua kozi ya makocha wa golikipa inayoendelea katika Uwanja wa Karume
jijini Dar es Salaam.
“Naishukuru
FIFA kwa kuipa Tanzania nafasi ya kuendesha mafunzo hayo ya makocha wa makipa
kwa mara ya kwanza nchini pia nawaomba washiriki wa kozi hii mtumie vema nafasi
kwa ajili ya kuendeleza mpira wa miguu”, alisema Said
Naye
mshiriki Mohamed Mwameja ‘Tanzania One’ ambaye amewahi kuidakia Simba na timu
ya Taifa alishukuru kupata kozi hiyo na kusema itawasaidia kujua makosa yao
kwani wamekuwa wakifundisha kwa uzoefu ambao waliupata wakati wakicheza.
“Sisi
tunafundisha kwa kutumia uzoefu tuliopata kutoka kwa waliotufundisha wakati
tukicheza hivyo kozi hii itatufanya tujitambue wapi tulikuwa tukikosea ili
turekebishe na tupate makipa bora”, alisema Mwameja
Jumla
ya makocha 31 wanashiriki kozi hiyo kutoka vilabu vyote viliyovopo Ligi Kuu ya
Tanzania Bara na Zanzibar na magolikipa wa zamani walio wahi kudaka timu za
Taifa.
Kozi hiyo
inaendeshwa na mkufunzi wa FIFA Elaxander kutoka nchini Ufaransa, ambaye
alidumu kama golikipa kwa miaka 20 na inatarajiwa kufungwa Julai 17, mwaka huu
No comments:
Post a Comment