Stars
ambayo imeweka kambi ya mazoezi takribani kwa wiki moja sasa jijini
Addis Ababa leo imeendelea na raiba yake ya mazoezi katika uwanja wa
Taifa, amabpo leo imefanya mazoezi yake asububuhi tu.
Kocha
mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema, anashukuru maendeleo ya kambi
ni mazuri timu yake inafanya mazoezi katika viwanja viwili vizuri
vilivyopo Addis Ababa, uwanja wa Taifa na uwanja wa Benki ya Biashara
ya Ethiopia.
Nooij
amesema amekuwa akiwafundisha wachezaji wake kucheza mpira wa kasi na
pasi za haraka haraka, jambo ambalo wachezaji wameonyesha kufuata vizuri
maelekezo yake na kusema wanamuelewa vizuri.
Akiongelea
mchezo dhidi ya Misri siku ya jumapili, Nooij amesema timu inakwenda
kupambana kusaka matokeo mazuri katika mchezo, nafahamu tunaenda cheza
ugenini, nimewaelekeza vijana wangu wanaocheza nafasi ya ushambuliaji
kutumia vizuri nafasi tutakazozipata katika mchezo huo.
Aidha
kocha Nooij amesema katika mpira hakuna kinachoshindikana, kambi ya
wiki moja Addis Ababa imewasaidia wachezaji kukaa pamoja na kushika
maelekezo yake vizuri, hivyo anaamini timu yake itafanya vizuri katika
mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON.
Katika
kikosi cha wachezaji wa 22 waliopo kambini jijini Addis Ababa hakuna
mchezaji majeruhi, wachezaji wote wako vizuri kiafya, kifikra na morali
ni ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo dhidi ya Mapharao.
Taifa
Stars inatarajia kuondoka kesho jioni ijumaa kuelekea nchini Misri kwa
shirika la ndege la Ethiopia majira ya saa 5 usiku na kufika Cairo
majira ya saa 8 usiku, kisha kuunganisha safari ya kuelekea jijini
Alexandria ambapo timu mchezo huo utakapofanyika.
Mchezo
kati ya Misri dhidi ya Tanzania utachezwa katika uwanja wa Borg El Arab
kuanzia majira ya saa 1 jioni kwa saaa za huku, sawa na saa 2 kamili
usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Waamuzi
wa mchezo huo wanatokea nchini Ethiopia ambapo ni Bamlak Tessema Weyesa
(mwamuzi wa kati), Kinfe Yilma (mwamuzi msaidizi wa kwanza), na Wolday
Hailerague (mwamuzi msaidizi wa pili).
NB: Picha za mazoezi ya Stars leo asubuhi uwanja wa Taifa - Addis Ababa zimeambatanishwa.
No comments:
Post a Comment