Mtanzania Emily Mgeta amesaini mkataba
wa mwaka mmoja kuichezea Neckarsulmer ya Ujerumani.
Mgeta aliyewahi kuichezea Simba,
amejiunga na klabu hiyo ya daraja la sita nchini humo.
“Nimesaini mwaka mmoja, nilifanya
majaribio na kufuzu na sasa naangalia namna nitakavyopambana,” alisema beki
huyo wa kushoto kutoka Ujerumani alipozungumza na SALEHJEMBE.
Mgeta ni mmoja wa vijana waliokuwa katika kikosi cha akina Said Ndemla, Ramadhani Singano ‘Messi’ na wengine.
Kwa hisani ya Saleh Jembe
No comments:
Post a Comment