Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, June 6, 2015

ANGEL DI MARIA: NITABAKI OLD TRAFFORD, SIENDI PSG


Licha ya kunyemelewa na Matajiri wa Klabu ya France Paris Saint-Germain, Winga kutoka Argentina Angel Di Maria amesema atabaki na Manchester United Msimu ujao.
Mchezaji huyo, ambae aliweka rekodi ya Dau kubwa la Uhamisho huko Uingereza alipohamia Manchester United kutoka Real Madrid Msimu uliopita, alishindwa kung'ara katika Msimu wake wa kwanza huko England.
Hilo limefanya Klabu nyingine nje ya England kumnyemelea na hasa PSG ambao ndio Mabingwa wa France.
Lakini, Di Maria, mwenye Miaka 27, na ambae kwa sasa yupo na Kikosi cha Argentina kinachojitayarisha na Copa America, amesema: "Nimemaliza Msimu wangu wa kwanza na Manchester United sasa nitacheza Copa America na kisha kurudi Manchester na kujitahidi kufanya vyema!"

Aliongeza: "Ulikuwa Msimu mgumu kwangu. Nadhani ilikuwa ngumu kwangu kwa sababu ni Nchi nyingine na ni Ligi nyingine na hii Ligi ni ngumu mno kupita ile ya Spain!"
"Nilishindwa kubadilika kama nilivyotaka. La Liga na Ligi Kuu England ni tofauti kabisa. Ligi Kuu England ina nguvu zaidi. Haikuwa rahisi. Nilibaki kucheza Dakika chache."

No comments:

Post a Comment