MONACO, Ufaransa
BEKI wazamani wa Chelsea amesema kuwa ushindi wa 3-1 wa
timu yake katika mchezo wa kwanza sio wakushangaza, lakini anakiri kuwa Monaco
bado haijajihakikishia nafasi ya kutinga robo fainali.
Beki wa Monaco Ricardo Carvalho alisema ushindi wao huo
wa 3-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Arsenal hauipi
nafasi ama Arsene Wenger au timu yake.
Kabla ya kucheza mchezo wa marudiano Jumanne, Carvalho – ambaye
alikuwa ameumia katika mchezo wa kwanza, alisema kuteleza kwa Arsenal ni sehemu
ya mchezo, na Monaco nao wanaweza kupoteza faida ya kucheza nyumbani katika
mchezo huo wa Jumanne.
"Sijui [kama Arsenal wanaidharau Monaco]. Sifikirii
hivyo," alisema beki huyo wa kati wazamani wa Chelsea. “Wakati fulani hilo hutokea
katika soka. Ni kweli, kwa wengi ni jambo la ajabu.
No comments:
Post a Comment