Huko Estadio El Madrigal Mjini Villareal, Barcelona waliichapa Villareal Bao 3-1 na kuitoa kwa Jumla ya Mabao 6-2 baada ya kuifunga Villareal 3-1 Uwanjani Nou Camp katika Mechi ya Kwanza.
Ushindi kwa Barca ulikuja Kipindi cha Pili kwa Bao za Luis Suarez na Neymar katika Dakika za 73 na 88.
Kwenye Mechi nyingine ya Nusu Fainali ambayo ilichezwa huko Estadi Cornella-El Prat, Mjini Barcelona, Wenyeji Espanyol walitandikwa 2-0 na Athletic Bilbao na kutupwa nje kwa Jumla ya Mabao 3-1.
Bao za Bilbao hapo Jana zilifungwa na Aritz Aduriz Zubeldia, Dakika ya 13, na Xabier Etxeita, Dakika ya 42.
Fainali ya Copa del Rey itachezwa hapo Mei 30 kati ya Barcelona na Athletic Bilbao kwenye Uwanja ambao bado haujathibitishwa.
No comments:
Post a Comment