Manchester United inasaka ushindi wake wa sita mfululizo kwenye Ligi Kuu England Jumapili Uwanjani Old Trafford kwa kuendeleza machungu kwa Liverpool ambayo ipo mrama Msimu huu.
Baada ya kuanza vibaya Msimu huu ukiwa ni mwendelezo wa Msimu uliopita walipomaliza Nafasi ya 7 wakati Liverpool iliukosa Ubingwa kidogo na kumaliza Nafasi ya Pili, Man United hivi karibuni imekaza uzi licha ya kukumbwa na majeruhi lukuki na Jumatatu iliyopita waliitandika Southampton Ugenini Bao 2-1 na kukamata Nafasi ya 3 ambayo mara ya mwisho kuishika ni Agosti 2013.
Msimu huu Liverpool wamedorora, wapo Nafasi ya 9 na Jumatano Usiku wametupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI huku kwenye Ligi wakiwa wameshinda Mechi 2 tu kati ya 6 walizocheza mwisho.
Straika wa Man United, Robin van Persie, ambae ndie aliefunga Bao zote zilizoizamisha Southampton na kabla Mechi hiyo kufunga Bao 1 na kunyamazisha wapondaji wake, amesema sasa Timu yao imerudi kwenye fomu.
Amesema: “Gemu ijayo ni na Liverpool, tunaingojea kwa hamu. Tuna furaha kwa sababu sasa tunapanda chati. Lazima tubakishe msukumo.”
Nao Vinara wa Ligi, Chelsea, baada ya kunyukwa kwa mara ya kwanza Msimu huu walipopigwa 2-1 na Newcastle Jumamosi iliyopita, watakuwa kwao Stamford Bridge Jumamosi kucheza na Hull City ambao wako Nafasi ya 3 toka mkiani.
Timu ya Pili kwenye Ligi, Man City, ambao ni Mabingwa Watetezi, watacheza Ugenini na Leicester City ambayo iko mkiani.
Mechi za Jumamosi zitahitimishwa na Mechi ya Uwanjani Emirates wakati Arsenal, ambayo ilichapwa na Stoke City Wikiendi iliyopita, watacheza na Newcastle inayotoka kwenye furaha ya kuwa Timu ya kwanza kuifunga Chelsea Msimu huu.RATIBA
Jumamosi Desemba 13
18:00 Burnley v Southampton
18:00 Chelsea v Hull City
18:00 Crystal Palace v Stoke
18:00 Leicester v Man City
18:00 Sunderland v West Ham
18:00 West Brom v Aston Villa
20:30 Arsenal v Newcastle
Jumapili Desemba 14
16:00 Man United v Liverpool
19:00 Swansea v Tottenham
Jumatatu Desemba 15
23:00 Everton v QPR
No comments:
Post a Comment