Tamko la Kundi hilo limesema: “United Reel lina Mashabiki walio hai kutoka kila Bara Duniani na tunaungana katika mapenzi yetu kwa Ronaldo kama Mchezaji na Mtu. Tuko pamoja na hatutapumzika mpaka tumrudishe Ronaldo Nyumbani.”
Ijumaa iliyopita, akiongea na Wanahabari, Meneja wa Man United Louis Van Gaal alijibu swali kwamba upo uwezekano wa wao kumchukua Ronaldo.
Van Gaal alisema: “Ndio lakini haya ni mazungumzo ya Magazeti na sidhani kama Vyombo vya Habari vitamnunua!”
Alipokazaniwa kujibu swali hilo, Van Gaal alisema: “Inawezekana. Nilisema hivyo hivyo kwa Falcao. Wachezaji kama Ronaldo wanaleta mambo mengi kwenye Timu lakini sidhani kama Real watamuuza!”
Ronaldo, mwenye Miaka 29, alitwaa Mataji 8 akiwa chini ya Meneja Sir Alex Ferguson na Mwaka 2009 aliuzwa kwa Real kwa Dau la Rekodi ya Dunia kwa wakati huo la Pauni Milioni 80.
Mwezi uliopita, Ronaldo, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani, alikiri angefurahia kurudi Man United pale aliposema: “Naipenda Manchester na huwezi kujua katika Soka. Ni kweli nina furaha hapa Real, ni nyumbani, ni Klabu yangu, lakini United walinitendea wema sana, na huwezi kujua!”
Aliongeza: “Bado nina mawasiliano na baadhi ya Watu huko kwa sababu nllikuwa na uhusiano mzuri na kila Mtu – ni kama Familia yangu ya pili!”
No comments:
Post a Comment