BAADA
ya Jana kuongoza Bao 3-1 huko King Power Stadium katika Mechi ya Ligi
Kuu England, Manchester United walijikuta wakibondwa 5-3 na Leicester
City huku Refa Mark Clattenburg akilaumiwa sana kwa Penati ‘tata’
iliyozaa Bao la Pili la Leicester City.
Hazikudumu
hata Dakika 2 baada ya Penati hiyo kutolewa, Leicester City
wakasawazisha na kisha kuongeza Bao 2 nyingine, moja likiwa la Penati
nyingine iliyosababisha pia Beki wa Man United Chipukizi Tyler Blackett
kupewa Kadi Nyekundu.
Wachambuzi huko England wamedai Penati iliyozaa Bao la Pili kwa Leicester ndiyo ilibadili Gemu na haikustahili kabisa.
Msimamo
huo umeungwa mkono na aliekuwa Refa mkubwa huko England, Graham Poll,
ambae alidai Refa Mark Clattenburg alikosea kabisa kuwapa Penati hiyo
Leicester City.
Poll
alidai Refa huyo alipaswa kutoa Rafu baada ya Fowadi wa Leicester,
Jamie Vardy, kumsukuma Rafael, na mbali ya hiyo, kitendo cha baadae ya
tukio hilo pale Rafael alipoinuka na kumkabili tena Vardy ambae safari
hii akajiangusha yeye, hakikustahili kabisa Penati.

Mbali
ya utata huo, Wachambuzi pia wamenyooshea kidole Difensi mbovu ya Man
United kwa kuruhusu Bao 3, ukiondoa hizo Penati mbili, za laini kabisa
katika Mechi ambayo ukweli waliitawala na kuwa na kila sababu ya
kushinda hasa baada ya kuwa Goli 3-1 mbele.
Pengine,
Man United watajutia sana kwa nini hawakusaini Madifendi maarufu
waliojengeka pamoja na Kiungo Mkabaji mkali katika Kipindi cha Usajili
wa Mwezi Julai.
Mwamuzi mwenyewe yupo nyuma..mpira upo mbele..kwa maana kama upo nje ya Uwanja! wakakausha!

Di Maria akiwa chini anajiuguza..baada ya kusukumwa nje na Refa kupeta..

Balaa lilianzia hapa...

2-3

4-3

5-3

Tyler Blackett alioneshwa Kadi nyekundu kwa rafu hii
No comments:
Post a Comment