Taarifa ya afisa habari na mawasiliano wa TFF Bonface Wambura imesema kuwa TFF inafanya Jitihada kumaliza deni hilo. Pia wanachunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo.
Tukio kama hilo liliwahi kutokea mwaka jana kama picha ya chini inavyoonekana
Pichani juu ni picha iliyopigwa mwaka jana ambapo kutokana na deni la malimbikizo ya malipo ya makazi ya waamuzi katika hoteli ya SAFINA waliochezesha michuano ya Chalenji mwaka 2011, ilipelekea basi dogo la shirikisho la soka nchini TFF walilopewa na NMB kufungwa mnyororo ndani viunga vya uwanja wa kumbukumbu ya Karume ambapo deni hilo lilifikia zaidi ya shilingi milioni 51.
Breakdown ya kampuni ya Flamingo Auction Mart linatekeleza amri ya mahakama ya Kivukoni Kinondoni ya kukamtwa kwa mabasi mawili likiwemo moja kubwa lililotolewa na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, deni hilo hatimaye lilimalizwa na sasa mahakama ina amrisha kukamatwa kwa basi kubwa kama ilivyo tolewa taarifa na msemaji wa TFF Bonface Wambura.
No comments:
Post a Comment