Didier Drogba akigumia maumivu |
Didier
Drogba huenda asirudi uwanjani katika kipindi cha miezi minne mpaka
sita kufuatia jeraha la kifundo alilolipata wakati wa mchezo wa
maandalizi ya msimu dhidi ya Ferencvaros Jumapili iliyopita.
Mshambuliaji
huyo wa 'The Blues' amekumbwa na jeraha hilo wakati akishuka chini
kutoka hewani akipiga mpira kichwa dakika ya 28 mchezo ambao Chelsea
ilishinda 2-1 huko Groupama
Arena mjini Budapest.
Huu ni mfano wa jeraha la Drogba |
Gazeti
la Marca la nchini Hispania limedai kuwa jeraha la Drogba linaweza kuwa
baya zaidi ya hapo awali kwani vipimo vinaonyeshwa kuwa mifupa
inayounganisha kikanyagio na kisigino imeachana.
No comments:
Post a Comment