Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, July 8, 2014

Nani wa kufa nani wa kupona kwenye nusu fainali kati ya Ujerumani au Brazil Jumanne na Argentina na Uholanzi? Historia itajiandika tena


Ni Brazil dhidi ya Ujerumani na Uholanzi dhidi ya Argentina katika nusu fainali , kesho(08.07.2014) na Jumatano, lakini Brazil imedhoofika kumkosa mshambuliaji nyota Neymar na Argentina itamkosa mchezaji muhimu Di Maria. 
Ujerumani kwa upande wake inawania kulipa kisasi dhidi ya kufungwa katika mchezo wa fainali 2002 dhidi ya Brazil.
Mlinzi Mats Hummels
 Wakati Brazil na Ujerumani zikijitayarisha kupambana katika mchezo wao wa nusu fainali kesho Jumanne, falsafa za zamani za soka katika nchi hizo zinaandikwa upya.
Cha kushangaza kwa mataifa hayo mawili vigogo katika kombe la dunia zikifikia kiwango cha nusu fainali mara 24, hii itakuwa mara yao ya pili kukutana katika kombe la dunia baada ya fainali ya mwaka 2002.
Wakati huo Ujerumani ambayo haikuwa katika kiwango cha juu kama ilivyo hivi sasa na ambayo ilipambana tu hadi kufika fainali kwa kupata ushindi wa bao 1-0 , wakisaidiwa na mlinda mlango wao maarufu wakati huo Oliver Kahn , walipambana na kikosi cha Brazil kilichokuwa kimesheheni washambuliaji hatari Ronaldo, Ronaldinho na Rivaldo.

Usiku huo mlinda mlango Oliver Kahn alifanya makosa na kukipa kikosi cha Luiz Felipe Scolari nafasi ya kunyakua taji lake la tano la kombe la dunia.
Scolari ndie amebakia
Hata hivyo jambo linaloweza kudokezwa tu hapa ni kwamba tangu timu hizo kupambana miaka 12 iliyopita ni scolari pekee ambaye bado yuko madarakani katika kikosi cha selecao Brazil na kwamba Ujerumani bado ina mlinda mlango hodari Manuel Neuer.
Ujerumani imekamilisha pasi 500 zaidi kuliko timu yoyote nyingine katika mashindano hayo na zaidi ya 1,000 kuliko ilivyofanya Brazil, ambayo bado iko nyuma ya Chile licha ya kucheza mchezo mmoja zaidi.

Nusu fainali ya kesho ni mpambano wa kiakili kwa Joachim Loew , ambaye ana hatari ya kuitwa mtu aliyekaribia kupata taji.
Baada ya miaka minane akiwa kocha wa Die Mannschaft , Loew hadi sasa ameifikisha timu hiyo katika nusu fainali moja ya kombe la dunia, fainali ya kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2008 na nusu fainali ya kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2012, hajaleta taji.
Ni muhimu kiasi gani kuwa watulivu katika pambano hilo kati ya Ujerumani na Brazil , mchezaji wa kati wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger amesema , mchezo huo ni changamoto kubwa kabisa.
"Hata uwe na uzoefu ama umecheza michezo mingi kiasi gani, mchezo kama huo unakuwa ni wa pekee , hususan dhidi ya wenyeji Brazil katika nchi kama hiyo ambayo ina wazimu wa kandanda na ambayo inajitambulisha kwa njia ya ajabu kabisa na kikosi hicho cha Selecao. Hali hiyo inaufanya mchezo huo kuwa na hamasa kubwa. Mtu anaufurahia , anauhisi mwilini na hupata burudani ya pekee katika mchezo kama huo."
Ujerumani itakumbana na Brazil ambayo imekuwa na mapambano ya nguvu zaidi wakati wenyeji hao wakijaribu kunyakua taji hilo bila ya nyota wao Neymar.
Brazil imelazimika kufanya mabadiliko bila ya mchezeshaji wa timu hiyo Neymar pamoja na Thiago Silva ambaye hatacheza kutokana na kuwa na kadi tatu za njano, wakati Selecao wanawania kutimiza ndoto ya kulinyakua kombe la dunia mara sita.
Bila Neymar Brazil si chochote?
Kocha msaidizi wa Ujerumani Hansi Flick amesema jana katika mkutano na waandishi habari kuwa kikosi chake kinafurahia changamoto hiyo.

"Ni timu ambayo ina wachezaji wa aina ya pekee, ambao wanauwezo wa kupambana mtu kwa mtu, katika mashambulizi na hata ulinzi. Baadhi ya nyakati hupitiliza hata mipaka iliyowekwa. Kwa hali hiyo tunatarajia licha ya kutokuwapo Neymar na Thiago Silva , kwamba kikosi hicho kitaweza kupata watu wa kujaza nafasi hizo na kufikia kiwango chao na kwetu sisi tutapambana na timu imara, hicho ndio tunachokitarajia."
Kutokana na hali hiyo katika mkutano huo na waandishi habari jana Jumapili, mchezaji wa kati wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger amesema mwamuzi Marco Rodriguez ni lazima aangalie sana wachezaji wa Brazil ambao watatumia nguvu kupita kiasi katika mchezo huo wa nusu fainali kesho na kuhakikisha faulo hazipiti bila kuadhibiwa.
Refa huyo kutoka Mexico , ambaye alikuwa mwamuzi katika mchezo ambapo mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez alimng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini, ameteuliwa kuamua mchezo huo wa nusu fainali mjini Belo Horizonte.

Brazil imeamua kukata rufaa dhidi ya kuzuiwa kwa Silva kucheza katika mchezo wa kesho , lakini ni mapambano ya kutumia nguvu zaidi yaliyoonekana sana katika mchezo huo wa robo fainali kutoka kwa wenyeji na Schweinsteiger hataki kurejewa kwa hali hiyo.
Katika duru ya makundi timu zilizotarajiwa kusonga mbele, nyingi zilifanya hivyo. Lakini katika awamu ya mtoano ya timu 16 , timu nyingi zilizopigiwa upatu kutoroka na kombe hilo zilipata taabu kuvuka kikwazo hicho. hivi sasa zimebaki timu nne.
Wabrazil wanaonekana kukata tamaa bila jogoo wao Neymar katika mchezo wa nusu fainali dhdi ya Ujerumani pamoja na nahodha wao Thiago Silva.
Willian na Bernard , wachezaji wawili ambao wanaweza kuchukua nafasi ya Neymar katika kikosi cha Barzil wamesisitiza jana kuwa kikosi chao kinaweza bado kushinda taji hilo la kombe la dunia bila ya nyota huyo.
Hata hivyo Ujerumani itabidi kupambana pia na uchawi pamoja na kikosi cha Selecao katika mchezo wa kesho wakati mtaalamu wa voodoo anapanga kufanya vitu vyake dhidi ya Die Mannschaft.
"Nitamchukua mchezaji wao nyota na kumfunga miguu ili asiweze kukimbia uwanjani," amesema Sillman , akimaanisha kutumia voodoo kumfunga mwanasesere ambaye atakuwa mchezaji ambaye hakutajwa jina wa Ujerumani hatua itakayofanyika kabla ya mchezo huo. Hivyo ni vituko kutoka huko Brazil.
Benchi la ufundi la Uholanzi likiongozwa na Van Gaal
Wachezaji wa Uholanzi wakipongezana
Van Gaal akimalizia maelekezo kabla ya Jumatano kuikabili Argentina

Argentina nayo yaikabili Uholanzi
Argentina na Uholanzi nazo zinamiadi siku ya Jumatano katika nusu fainali ya pili ya kombe la dunia, ikiwa ni miaka 36 tangu timu hizo zikutane katika fainali iliyokuwa na utata mwaka 1978 mjini Buenos Aires nchini Argentina.
Kombe la dunia lililochezwa chini ya utawala wa kidikteta ulimalizika kwa wenyeji kuwapa kipigo Uholanzi cha mabao 3-1 baada ya muda wa nyongeza, ambapo Mario Kempes alipachika wavuni mabao 2.
Kwa Wadachi , Uholanzi , ni kipigo cha pili katika fainali, baada ya kufungwa mabao 2-1 na Ujerumani magharibi katika fainali ya mwaka 1974, lakini hakuna timu kutoka Ulaya ambayo imefika karibu kulinyakua kombe hilo katika ardhi ya America kusini.

No comments:

Post a Comment