Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 5, 2014

Liverpool wastukia kamtego ka Barcelona juu ya Suarez, wagomea mpango wa kubadilishana na Sanchez


Alexis Sanchez kubadilishwa na Suarez
Majogoo wa jiji la London Liverpool wamelikataa ombi la viongozi wa FC Barcelona ambao tangu jana wapo nchini Uingeereza kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Uruguay Luis Alberto Suarez Diaz.

Liverpool FC wamewagomea viongozi wa Barcelona katika mazungumzo yanayo endelea mjini Liverpool ambapo Barca wanahitaji kufanya dili la kumtoa mshambuliaji wa pembebni kutoka nchini chile Alexis Sanchez pamoja na kiasi cha pesa ili wakamilishiwe mpango wa kumsajili Suarez.

Liverpool wamesisitiza kuwa hawako tayari atayari kuona dili hilo linafanikiwa kama viongozi wa Barcelona wanavyohitaji, na badala yake viongozi wa The reds wamesema wanahitaji pesa taslim zisizopungua paund million 80.

Hata hivyo viongozi wa Barcelona wamekubaliana na msisitizo huo, lakini wamekiri kuwa na kiasi cha paund million 70, ambazo wanaamini zitatosha katika mpango wa kumsajili Suarez ambaye kwa sasa anatumikia adhabu ya kutojihusisha na soka kwa kipindic ha miezi minne kufutaia kosa la kumng’ata kwa makusudi Giorgio Chiellini wa timu ya taifa ya Italia.

Kukubalia kwa viongozi wa FC Barcelona kutoka kiasi cha paundi million 70, kutoa mwanya kwa viongozi wa klabu ya Arsenal kujipanga vizuri kwa lengo la kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Chile Alexis Sanchez ambaye nahusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na The Gunners.

Inadaiwa tayari Arsenal wameshawasilisha ofa ya paund millioni 32 huko Camp Nou, kwa lengo la kumsajili Sanchez ambaye ameshaambiwa hayupo kwenye mipango ya meneja mpya wa FC Barcelona Luis Enrique.

No comments:

Post a Comment