Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 21, 2014

VAN PERSIE NJE WIKI 6 KWA MAJERAHA YA GOTI, KUIKOSA MITANANGE NANE. PIGO ZITO KWA UNITED!!


Straika wa Man United, Robin van Persie atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi moja na kukosa mechi nane za timu yake kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya Goti.
Rooney na Van Persie
Van Persie ambaye alifunga hat trick iliyoipeleka Man United hatua ya robo fainali alitolewa nje na machela katika mchezo huo katika dakika za mwisho za huo, na leo hii baada ya kufanyiwa vipimo kiundani imegundulika amepata majeruhi yatakayomuweka nje kwa muda wa wiki 4-6.
Kwa maana hiyo mdachi huyo ataukosa mchezo dhidi ya Manchester City pamoja na mchezo wa kwanza wa robo fainali ya UCL dhidi ya Bayern Munich, hivyo kuiachia timu yake pigo zito.
OOOOhhhhhh!! Van Persie akishangilia siku hiyo kabla kuumia hakujamkuta!Van Persie akishangilia moja ya bao lake siku hiyoRooney na Van Persie wakipongezana
Hapa alipongezwa baada ya kufunga Hat-trick

Robin van Persie alitolewa nje nje kwa machela baada ya kuumia kwenye mtanange na Olympiacos kwenye Uefa Champions Ligi. "Kufuatia uchunguzi wa kina, Robin van Persie ameumia goti, ambalo litamuweka nje kwa kiasi cha wiki nne hadi sita,".
Pamoja na kukosa mechi dhidi ya West Ham na Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Van Persie, ambaye amefunga mabao 17 msimu huu, atakosa pia mechi dhidi ya Manchester City Jumanne.

Wayne Rooney akiwa karibu na Van Persie

Van Persie ......pole sana, Kwa machungu mshambuliaji wa Manchester United akitolewa nje huku mwenzie Rooney akiwa kwenye maswali mazito....kujiuliza..
MITANANGE ATAKAYOKOSA: 
Mar 23: West Ham (A)
Mar 25: Man City (H)
Mar 29: Aston Villa (H)
Apr 1: Bayern Munich (H)
Apr 5: Newcastle (A)
Apr 9: Bayern Munich (A)
Apr 20: Everton (A)
Apr 26: Norwich (H)

No comments:

Post a Comment