Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 13, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BARCELONA 2 v MANCHESTER CITY 1 (Agg.4-1) LIONEL MESSI NA DANIEL ALVES WAIPATIA USHINDI BARCA NDANI YA NOU CAMP!! CITY WATUPWA NJE!

Kikosi cha Barcelona kilichoanza.
FC Barcelona vs Manchester City, Mtanange wa kipindi cha kwanza unamalizika wa dakika 45 wakiwa bado 0-0, Hakuna cha Barca wa City, Barcelona wakijaribu mara kwa mara kuingia kwenye eneo la hatari la City bila kufunga, Neymar na Messi wakikosa mabao.Joe Hart gets out quickly to save at the feet of Lionel Messi. Wao City nao wamejaribu kuingia lakini shuti lililopigwa na Nasri lilidakwa na Kipa wa Barca. Kumbuka katika Mtanange wa kwanza walitoka 2-0 huko Etihad na sasa Man City wanataka kupindua kipigo hicho cha bao hizo mbili na kuwatupa nje Barcelona kwenye uwanja wao Nou Camp.Messi na Aguero wakioneshana ubabe!
Kipindi cha pili dakika ya 67 Lionel Messi akaipachikia bao Barca baada ya mabeki wa City kujichanganya. Lescott akituliza mpira bila umakini na hatimae Messi kuuchukua na kutupia nyavuni. Dakika ya 78 Mchezaji wa City  Pablo Zabaleta anaonshwa kadi ya njano na nyekundu na kutolewa nje ya uwanja baada ya kufanya ndivyo sivyo na Mwamuzi S. Lannoy‎ kumtoa nje. Dakika ya 80 Barca walifanya mabadiliko Neymar alitoka na nafasi yake ilichukuliwa na Alexis Sánchez. Dakika za lala salama dakika ya 89 kona ilipigwa na hatimae Vincent Kompany akasawazisha bao kwa kufanya 1-1(Agg.3-1) na hapo hapo kwenye dakika za majeruhi dakika za nyongeza Barcelona walifanya mashambulizi na kupachika bao la pili kwa kufanya 2-1 (Agg. 4-1) Bao lililofungwa na Daniel Alves akipewa pasi safi na Andrés Iniesta Luján ndani ya box na kuachia shuti kali hadi ndani ya lango la City na mpira kumalizika. Ushindi huu wa Barca unawaondosha City nje ya  michuano hii ya Uefa kwenye hatua ya 16 bora, Huku Barca wakisonga mbele kwenye hatua ya robo fainali.Kocha wa City kautazamia kwa mashabikiYaya Toure na pique wakichuana vikali Silva akiupoza mpiraIniesta mbele ya Vicent KompanyHapa hukatizi ndugu yangu ....hapa ni Nou Camp!Chupu chupu hapa Vicent Kompany kidogo awapige bao la kichwa..katika kipindi cha kwanza.Kidogo!!Lescott akipitwa na Lionel MessiNeymar baada ya kukosa bao la wazi hapa!!Neymar akionekana kuumia kukosa bao!Mtu kati...Daniel Alves akichuana hapa ...nivute ni kuvute na David SilvaNeymar akiendesha...Utakubali tuu!Messi na LescottPicha mbali .....kaa pembeni!!Nani fundi hapa!Neymar kwenye patashika na wachezaji wa City!Hoi!!! msaidizi wa kocha wa City Ruben Cousillas Unakosa!!tutajutia baadae......Benchi halikukalika!!!Kocha wa England Roy Hodgson nae yupo Spain live kuangalia kipute cha vijana wake wanaokipiga katika timu ya Taifa, Na hapa alikuwa akiteta jambo na kupeana salama na Manuel Pellegrini wa City pamoja na viongozi wengine kwenye uwanja wa Nou Camp.

VIKOSI:
Barcelona:
Valdes, Dani Alves, Pique, Mascherano, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Messi, Fabregas, Neymar.
Subs: Pinto, Pedro, Alexis, Bartra, Song, Adriano, Sergi Roberto.
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Lescott, Kolarov, Silva, Fernandinho, Milner, Nasri, Toure, Aguero.
Subs: Pantilimon, Negredo, Dzeko, Javi Garcia, Jesus Navas, Clichy, Boyata.
Referee: Stephane Lannoy (France)

No comments:

Post a Comment