Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, March 26, 2014

ARSENAL 2 v SWANSEA CITY 2, MATHIEU FLAMINI AJIMALIZA MWENYEWE KWA KUJIFUNGA BAO NA KUWEKA SARE KWENYE DAKIKA ZA LALA SALAMA EMIRATES!!

Arsenal wamepata pigo tena usiku huu baada ya kutoka sare ya bao 2-2 na Swansea City Emirates usiku huu baada ya kukubali sare hiyo wakijifunga wao wenyewe kwenye dakika za mwishoni. Swansea ndio walioanza kuifunga bao Arsenal katika dakika ya 11 kupitia kwa Wilfried Bony kipindi cha kwanza.
Arsenal walitarajiwa kuzinduka na kushinda Mechi waliyocheza kwao Emirates na kweli walitanguliwa kwa Bao moja na Swansea City hadi Mapumziko na kujibu mapigo Kipindi cha Pili na kufunga Bao 2 ndani ya Dakika moja lakini mwishowe waliimwaga Mechi baada kujifunga wenyewe katika Dakika ya 90.

Bao hilo la kusawazisha la Swansea City lilifungwa mwishoni baada kizaazaa Golini ambapo Leon Britton alitanga kufunga na Beki Per Mertesacker kumzonga na Mpira kumgonga Kipa Wojciech Szczesny na kumbabatiza Kiungo Mathieu Flamini na kutinga wavuni. 
Hili ni pigo jingine kwa Arsenal katika kusaka Ubingwa Msimu huu kwani wamenasa Nafasi ya 4.Rosicky wa Arsenal akipelekeshana na Wilfried Bony wa Swansea 
Mathieu Flamini dhidi ya Ashley Williams wa Swansea City
Da!!! Majanga jamani!!!! kila mchezaji akiwa hana hamu!!! Emirates
Wilfried Bony mambo safi kwake!!!

No comments:

Post a Comment