Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 7, 2013

MBWANA SAMATA MCHEZAJI BORA WA MCHEZO WA UGANGA NA KILIMANJARO STARS LEO

Na Mahmoud Zubeiry, Mombasa
MSHAMBULIAJI wa Tanzania Bara, Mbwana Ally Samatta ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa Robo Fainali ya Kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge dhidi ya Uganda, The Cranes ambayo timu yake ilishinda kwa penalty 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Manispaa, Mombasa.
Wazi Samatta amepewa tuzo hiyo inayoambatana na zawadi ya king’amuzi na kifurushi GOtv kwa sababu ya kusababisha mabao yote mawili ya Stars yaliyofungwa na Mrisho Ngassa. 
Mbwana Samatta amekuwa mchezaji bora dhidi ya Uganda

Katika mchezo huo uliochezeshwa na Wish Yabarow wa Somalia, aliyesaidiwa na KInde Mussa wa Ethiopia na Mohamed Idam wa Sudan, hadi mapumziko Stars ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-1.
Mshambuliaji wa Gor Mahia ya Kenya, Dani Sserunkuma alitangulia kuifungia Cranes bao dakika ya 16, baada ya kupokea krosi ya Hamisi Kiiza aliyemtoka Erasto Nyoni na kufumua shuti la chini lililompita kipa Ivo Mapunda.  
Dakika mbili baadaye, Mrisho Ngassa aliisawazishia Stars baada ya kuwazidi ujanja na maarifa ya kisoka mabeki wa Uganda, akimalizia mpira uliopigwa na Mbwana Ally Samatta.
Mshambuliaji huyo wa TP Mazembe ya DRC, aliangushwa chini nje kidogo ya eneo la hatari na mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa akaenda kupiga mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja kuipatia Stars bao la pili.
Baada ya bao hilo, Stars waliendelea kuishambulia Uganda kwa kujiamini zaidi, lakini mabeki wa Cranes walisimama imara kutoruhusu mabao zaidi.
Kipindi cha pili, Stars ilipata pigo dakika ya 53 baada ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kutolewa nje kwa nyekundu kwa kumchezea rafu Sserunkuma.
Uganda ikapata bao la kusawazisha dakika ya 73 kupitia kwa Martin Mpuga, aliyeunganisha kona ya Godfrey Walusimbi.
Kipa Ivo Mapunda alikuwa shujaa baada ya kuokoa penalti mbili za Dani Sserunkuma na Khalid Aucho wa Uganda na kuipa Stars ushindi wa penalti 3-2 baada ya sare ya 2-2 ndani ya dakika hizo 90.
Mbali na kuokoa penalti hizo mbili, Uganda walipoteza penalti nyingine moja baada ya Godfrey Walusimbi kupiga, wakati Hamisi Kiiza Emannuel Okwi ndiyo pekee walioifungia Cranes penalti.
Waliofunga penalti za Bara ni Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’na Erasto Nyoni, wakati Mbwana Samatta na Amri Kiemba walikosa.
Kwa matokeo hayo, Stars inarudia kuingia Nusu Faniali kama mwaka jana, wakati Uganda wanaacha taji Mombasa na kurejea nyumbani, Kampala.     
Aidha, Samatta anakuwa mchezaji wa pili wa Stars kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mechi, baada ya awali Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kushinda pia tuzo hiyo katika mchezo wa makundi dhidi ya Zambia, timu hizo zikitoka sare ya 1-1.

Kwa hisani ya Bin Zubeiry

No comments:

Post a Comment