RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi ameunda kamati mbili maalumu kwa ajili ya kutathmini muundo wa
ligi na kupendekeza namna ya kuboresha.
Pia kamati hizo
zitatathmini muundo wa Bodi ya Ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha
ikiwemo kuunda kampuni ambayo itakuwa na kazi ya kusimamia/ kuendesha ligi.
Akizungumza na wandishi wa habari, Ofisa Habari wa
Shirikisho la Soka nchini (TFF) Boniface Wambura ambaye pia ni Kaimu Katibu
Mkuu, alisema kuwa Kamati ya Kutathmini Muundo wa Ligi inaongozwa na Kocha wa
zamani wa Taifa Stars, Dk. Mshindo Msolla wakati Katibu ni Ofisa Mashindano wa
TFF, Idd Mshangama. Wajumbe ni Rahim Kangezi, Amri Said, Sunday Manara, Salim
Bawazir na Lucas Kisasa.
David Nchimbi kutoka Delloitte ndiye anayeongoza
Kamati ya Muundo wa Bodi ya Ligi wakati wajumbe ni Edwin Kidifu (Mwanasheria wa
SUMATRA), Jones Paul (Mkurugenzi wa Sunderland/Symbion Academy), Evans Aveva,
John Jambele, Masoud Sanani na Pelegrinius Rutahyuga.
Pia Rais Malinzi amemteua Pelegrinius Rutahyuga kuwa
Mshauri wa Rais kwenye masuala ya Ufundi
wakati Mshauri wa Rais kwenye
mambo ya Utawala atateuliwa baadaye.
Wakati huo huo jopo la wataalamu 20 walioteuliwa na Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi linakutana
kupanga mkakati wa kuonesha jinsi Tanzania inavyoweza kushiriki Fainali za
Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwaka 2015 nchini Morocco.
Kikao hicho
maalumu (retreat) kitafanyika mjini Zanzibar kuanzia Desemba 6-8 mwaka
huu chini ya Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali
mstaafu Idd Omari Kipingu.
Wengine ni makocha
Dk. Mshindo Msolla, Peter Mhina, Ayoub
Nyenzi, Abdallah Kibaden, Pelegrinius Rutahyuga, Kidao Wilfred, Salum Madadi,
Juma Mwambusi, Ken Mwaisabula, Boniface Mkwasa, Fred Minziro, Meja Abdul
Mingange, Ally Mayay na Dan Korosso na wajumbewengine toka Chama cha Mpira wa
Miguu Zanzibar (ZFA).
No comments:
Post a Comment