Kanda kabongo akimuhuumia Japhert Kaseba |
Bondia Omari Nampekecha 'peche boy' kushoto akipambana na hasani Kiware wakati wa mpambano huo nampekecha alishinda kwa pointi |
Bondia Pendo Njau kushoto akiwa na bondia Llulu Kayage wakati wa mpambano huo
Wapiganaji wa mpambano wa Kick Boxing Kareem Kutch (kushoto) akipambana na Hassani Juma 'Tata Boy' wakati wa mpambano huo kutch alishinda kwa pointi |
Wapiganaji wa mpambano wa Kick |
BONDIA Japhet Kaseba juzi alitawazwa kuwa
bingwa wa Taifa baada ya kumpiga kwa KO bondia Alibaba Ramadhan wa Arusha
kwenye raundi ya nne katika pambano lililokuwa la raundi 10 lililofanyika
Ukumbi wa Friends Corner Manzese, Dar es Salaam.
Kaseba
ambaye awali alikuwa akipigana ngumi na mateke kabla ya kuhamia kwenye ngumi tu
alionyesha umahiri wake wa kupiga makonde mazito ambayo yalionekana kumwelemea
Alibaba.
Katika kuonyesha kuwa yeye yupo fiti
Kaseba aliendelea kumrushia makonde mfululizo mpinzani wake na kusalimu amri
katika raundi ya nne.
Katika pambano la ngumi na mateke (Kick Boxing) Kareem kutch alimshinda kwa pointi
Hassan Juma 'Tata Boy’ kwenye pambano la raundi nne.
Akizungumza baada ya pambano hilo,
Japhet Kaseba alisema kuwa anashukuru kwa kumpiga Alibaba Ramadhan na kufanikiwa
kupata mkanda wa Ubingwa Taifa.
“Nashukuru Mungu kwa kutwaa ubingwa wa
Taifa hivyo mkanda huu unanipa chachu ya kuendelea kujifua vema ili kugombea
mikanda mingine”, alisema Kaseba.
Naye mwandaaji wa pambano hili
Mkurugenzi wa BigRight Promotion, Ibrahim
Kamwe aliwashukuru wadau wa ngumi kwa kumuunga mkono kwa wingi kwani
bila wao asingeweza kuandaa pambano hilo.
“Nawashukuru mabondia wote na wadau kwa
kunipa sapoti kwani bila wao nisingeweza kuandaa mapambano haya hivyo nawaomba waendelee kutusapoti kwani kwa
kufanya hivyo wanausadia mchezo wa masumbi”, alisema Kamwe
No comments:
Post a Comment