Kwa mujibu wa
chanzo chetu, wasanii hao wamebeba mimba hizo kwa nyakati tofauti na
wamekuwa wakijificha kukwepa aibu ya kubeba ujauzito kabla ya kufunga
ndoa.
Belina Mgeni.
“Wanaona aibu kubeba ujauzito kabla ya ndoa, wamekuwa wakijificha na
mbaya zaidi hawataki kujionesha maana wengi wao hawajawatambulisha
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mapaparazi wetu waliingia mzigoni
kusaka ukweli wa habari hiyo ambapo jitihada zilizaa matunda kwa
kupatikana kwa picha za mastaa hao zikionesha tayari vitumbo ndii.
Jennifer Kyaka ‘Odama’.
Baadhi yao, picha zilionesha mimba zikiwa ni kubwa huku wengine zikionekana ndiyo bado changa.
Aunty Lulu, Belina walionekana dhahiri kuwa ni waleo au kesho,
matumbo yao yalionekana ‘live’ ni makubwa, Odama yeye ilionekana bado
halijajitokeza vizuri.
Recho Haule.
Kwa upande wa Recho Haule, rafiki wa karibu aliyeomba hifadhi ya
jina, alipenyeza habari kuwa mimba aliyonayo shosti wake huyo ni ya
mpenzi wake wa kitambo, Saguda George lakini naye amekuwa akijifungia
ndani kukwepa macho ya watu.
“Recho ni mjamzito lakini amekuwa akijificha kukwepa kamera za
mapaparazi si unajua tena uchumba wake na Sagunda kila mmoja alikuwa
akiufatilia magazetini!”
Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Baada ya mapaparazi wetu kujitosheleza na ushahidi wa picha, zoezi la
kuwasaka wasanii hao ili kujua wahusika wa mimba hizo lakini simu zao
ziliita muda mrefu bila kupokelewa.
Baadhi ya mashabiki walioongea na paparazi wetu, hawakusita kuonesha
hisia zao kwa mastaa hao, kila mtu alikuwa na mtazamo wake juu ya mastaa
hao.
“Unajua kama Belina naona amebeba mimba ila yuko kwenye process ya
kufunga ndoa ingawa sijui ni lini kwani niliwahi kumsikia akisema kuwa
anaweza kufunga ndoa soon” alisema shabiki mmoja, mwingine akasema hivi:
“Sisi tujuavyo kioo cha jamii maana yake ni mtu kufanya yale
yanayofaa kuigwa lakini kwa hawa mastaa wetu wamefanya tofauti, wote
wamebeba mimba bila ndoa, sasa jamii itajifunza nini kutoka kwao?”
No comments:
Post a Comment