KIKOSI cha Afrika Kusini (Basetsana) kwa ajili ya
mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20
dhidi ya Tanzania (Tanzanite) kinatua nchini leo
Afrika Kusini itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) itatua saa 8 kamili mchana kwa ndege ya South Africa
Airways.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Ofisa Habari wa
Shirikisho la Soka nchini (TFF) Boniface Wambura ambaye pia ni Kaimu Katibu
Mkuu, alisema kuwa kuwa taarifa ambayo imetumwa na shirikisho la soka la Afrika
Kusini inasema kuwa msafara huo utakuwa na watu 25, wachezaji wakiwa 20.
Wachezaji wanaunda kikosi cha Basetsana ni makipa
Kaylin Swart, Regirl Ngobeni na Juliet Sethole. Mabeki ni Abongile Dlani, Caryn
van Reyneveld, Chamelle Wiltshire, Meagan Newman, Nomonde Nomthseke, Tiisetso
Makhubela na Vuyo Mkhabela.
Viungo ni Amanda November, Amogelang Motau, Gabriella
Salgado, Koketso Mamabolo, Nomvula Kgoale na Thembi Kgatlane na washambuliaji
ni Mosili Makhoali, obyn Moodaly, Sduduzo Dlamini na Shiwe Nogwanya.
Pia amesema viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa
Jumamosi ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange, sh. 2,000
kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.
Wambura
amewaomba watanzania kufika kwa wingi kuishangilia Tanzanite ili kuwapa moyo
waweze kukata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika fainali za Kombe la Dunia kwa
wasichana yanayotarajiwa kufanyika nchini Canada mwakani.
No comments:
Post a Comment