Raundi
ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambayo ipo katika raundi yake ya 12
inaendelea kesho (Novemba 2 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa
katika miji minne tofauti.
Mgambo
Shooting na Coastal Union zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga, Mbeya City na Ashanti United zitaumana kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex,
Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu,
Morogoro).
Raundi
hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Tanzania
Prisons itakuwa mwenyeji wa Oljoro kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7
mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashanti United vs
Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, na Ruvu Shooting vs Mtibwa
Sugar.
Novemba
7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa
Tanzania Prisons.
No comments:
Post a Comment