Javier Hernandez amedokeza anaweza kuihama Manchester United ikiwa hatapata nafasi ya kucheza.
Chicharito hakucheza Jumamosi huko
Craven Cottage wakati Man United inaifunga Fulham 3-1 kwenye Ligi Kuu
England licha ya kufunga Bao 2 wakati Man United ipoifunga Norwich City
kwenye Capital One Cup katikati ya wiki iliyopita. Jana Jumapili, Chicharito alitumia Mtandao wake wa Twitter kusambaza Makala ya Sky Sports iliyomnukuu Mchezaji mwenzake wa Timu ya Taifa ya Nchi yao Mexico, Carlos Vela, akimtaka Chicharito atafakari hatima yake hapo Manchester united.
Lakini baadae, Chicharito alifuta posti hiyo kwenye Twitter.
Msimu huu Chicharito amefunga Bao 4 katika Mechi 4 alizoanza lakini kwenye kupewa namba na Meneja David Moyes yuko nyuma ya Robin van Persie na Wayne Rooney
Vela, ambae alikaa Arsenal Miaka 7 na pia kuwa akikosa namba, amemuonya Chicharito kuwa anapaswa kuondoka Man United ikiwa hali yake haitabadilika.
Vela ameripotiwa kusema: “Javier ni Rafiki yangu mzuri na natumai atapata nafasi nyingi zaidi Man United. Yeye ni mmaliziaji mzuri sana huko England na nategemea Meneja mpya atampa nafasi zaidi. Kama akicheza mara kwa mara atafunga tu lakini sielewi Mchezaji mzuri kama yeye hachezi Mechi nyingi zaidi. Kama hachezi mara kwa mara itabidi afikirie kuondoka.”
Mchezaji wa zamani wa Arsenal Carlos Vela anayemshawishi kuikacha
United Chicharito kama nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza ni tete!!
No comments:
Post a Comment