Kocha
wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson anasisitiza kwamba
hatazingatia kurejea katika shughuli za ukocha wa kandanda.
Manchester
United hivi sasa wanashikilia nafasi ya 12 katika Ligi Kuu ya England
chini ya uongozi wa David Moyes, aliyeshikilia nafasi hiyo baada ya
Ferguson kustaafu mwishoni mwa msimu uliopita. "Mimi sina hamu ya kuwa meneja tena ,na kujisumbua roho yangu ," alisema Ferguson. "United wako mikononi mwa uongozi mzuri. David atakua poa. Ni meneja mzuri."
Ferguson, mwenye umri wa miaka 71, alidokeza kwamba Roman Abramovich alimtaka aiongoze Chelsea alipoinunua mnamo mwaka 2003.
"walimtuma wakala aniulize Abramovich alipochukua madaraka kwa mara ya kwanza ya klabu hiyo lakini niliwaambia 'Ng'oo."
Fergie kama anavyotambulika zaidi anasema alimwambia wazi Abramovich hakuna nafasi ya yeye kujiunga na Chelsea kwa kuwa alikuwa na Timu bora na yenye uchu wa kupata mafanikio.
No comments:
Post a Comment