Timu ya Taifa ya England
jana waliifunga Moldova 4-0 na kujikita kileleni mwa Kundi H la kuwania kucheza
Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwakani lakini Kocha wao, Roy Hodgson,
amekasirishwa sana na Refa kutoka Slovakia kwa kumpa Kadi ya Njano Danny Welbeck
itakayomfanya aikose Mechi muhimu sana ya Jumanne huko Kiev dhidi ya Ukraine.
Refa Ivan Kruzliak kutoka Slovakia kumpa Kadi ya Njano kwa kuendelea kucheza Mpira na kupiga shuti baada ya kupigwa Filimbi ya yeye kuotea kufuatia Bendera ya Msaidizi wa Refa kuashiria Ofsaidi ambayo hakika haikustahili.
Kocha Roy Hodgson alimvaa Refa wa Akiba na kumpandishia na Sekunde chache baadae Welbeck akaifungia England Bao la tatu na la kwanza kwake.
Mbali ya Hodgson kulalamika, hata Welbeck mwenyewe alimfuata Refa na kulalamika sana kuhusu Kadi ile.
Nae Hodgson alieleza: “Sidhani kama wapo Watu wengi, hata Marefa wenyewe, watakaounga mkono Kadi ile. Hata Kadi ya Njano ya kwanza aliyopewa Welbeck huko Montenegro Mwezi Machi ni uonevu kwani yeye alistahili Penati na si Kadi kwa kujiangusha. Sasa yupo nje Gemu ya Ukraine”
Upungufu huo, pamoja na kuwakosa Wayne Rooney na Andy Carroll, ambao ni Majeruhi, kunamfanya Hodgson amtegemee Jermaine Defoe, ambae nae ndio anarudi toka kwenye maumivu, na Rickie Lambert wa Southampton ambae Jana alicheza vizuri mno na kufunga Bao moja.
Pia upo uwezekano mdogo kwa Straika wa Liverpool, Daniel Sturridge, kusafiri kwenda Kiev ikiwa kesho Jumapili Madaktari watampasisha kupona kwake maumivu ya Paja ambalo yalimfanya Juzi arudi Klabuni kwake Liverpool kwa matibabu zaidi.
MSIMAMO:

KUNDI H | |||||||||
NAFASI | Team | P | W | D | L | F | A | GD | Pts |
1 | England | 7 | 4 | 3 | 0 | 25 | 3 | 22 | 15 |
2 | Montenegro | 8 | 4 | 3 | 1 | 15 | 8 | 7 | 15 |
3 | Ukraine | 7 | 4 | 2 | 1 | 19 | 4 | 15 | 14 |
4 | Poland | 7 | 2 | 4 | 1 | 13 | 8 | 5 | 10 |
5 | Moldova | 8 | 1 | 2 | 5 | 4 | 15 | -11 | 5 |
6 | San Marino | 7 | 0 | 0 | 7 | 0 | 38 | -38 | 0 |
KUMBUKA:
:WASHINDI 9 WA MAKUNDI WATATINGA MOJA KWA MOJA
BRAZIL
:WASHINDI WA PILI 8 BORA KATIKA MAKUNDI 9
WATAPANGIWA MECHI SPESHO ZA MCHUJO ZA MTOANO ILI KUPATA TIMU 4 KUUNGANA NA
WASHINDI 9 WA MAKUNDI KWENDA BRAZIL
RATIBA:
Jumanne Septemba 10
San Marino v
Poland
Ukraine v
England
Ijumaa Oktoba 11
England v
Montenegro
Moldova v San
Marino
Ukraine v
Poland
Jumanne Oktoba 15
England v
Poland
Montenegro v
Moldova
San Marino v
Ukraine
No comments:
Post a Comment