Naggi aliwasili klabuni hapo jumatatu iliyopita, kuchukua
nafasi ya Lawrence Mwalusako, ambaye
alikuwa akiikaimu nafasi hiyo kwa muda, baada ya uongozi mpya wa klabu
hiyo kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa awali Celestine Mwesigwa.
Akizungumza na leo jijini Dar es Salaam, Makamu
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga alisema hawataki kulumbana na wazee,
isipokuwa msimamo kamili wa uongozi kuhusiana na suala hilo watautoa leo.
"Tulitoa tenda kwa Kampuni moja, ambayo ilimpata Naggi
aliyekidhi sifa na vigezo, kupitia mchakato
kwa waombaji walioomba ajira hiyo, ambapo uraia siyo kigezo cha
kumuondoa huyo, kwani ni nafasi ya kuajiriwa.
"Bado hajaanza kazi rasmi kama inavyoelezwa na alienda
klabuni kwa ajili ya kumsalimia Lawrence Mwalusako, ambaye ni rafiki yake wa
muda mrefu," alisema Sanga
Alisema atakuwa Katibu rasmi pale tu watakapotoa taarifa za
kumtambulisha, lakini sasa bado hajashika madaraka hayo, ambayo yanafanywa na
Mwalusako.
Hata hivyo kauli hiyo inapingana na kauli aliyoitoa jumanne
iliyopita Katibu wa sasa Mwalusako, ambaye alinukuliwa kwenye vyombo vya habari
akisema tayari ameshaambiwa na uongozi wake amkabidhi madaraka Mkenya huyo.
Ambapo alisema ajira yake hiyo ilikuwa ya muda, wakati
viongozi wakiwa kwenye mchakato wa kumpata Katibu mpya.
Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali
alitoa tamko juzi jijini Dar es Salaam, ambapo alisema wanapinga ajira hiyo ya
Mkenya, kwani katiba yao inataka kiongozi yoyote lazima awe mwanachama waklabu
hiyo.
No comments:
Post a Comment