REAL Madrid wamekamilisha rasmi taratibu za kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs, Gareth Bale.
Kusajiliwa
kwa mchezaji huyo kunamfanya aungane na straika bora kabisa wa Madrid, Cristiano
Ronaldo, katika kusukuma mashambulizi ya timu hiyo.
Hali
hiyo itaifanya timu hiyo kuwa na muungano hatari zaidi kwenye safu ya
ushambuliaji, kutokana na wawili hao kuwa na rekodi zinazokaribiana.
GARETH
BALE
Namba
ya jezi: 11
Nafasi:
Kiungo mshambuliaji
Umri:
Miaka 24
Kuzaliwa:
Julai 16, 1989
Alikozaliwa:
Cardiff, Wales
Urefu:
Futi 6 inchi 1 (1.83m)
Uzito:
Kilo 74
****
CRISTIANO
RONALDO
Namba
ya jezi: 7
Nafasi:
Mshambuliaji
Umri:
Miaka 28
Kuzaliwa:
Februari 5, 1985
Alikozaliwa:
Madeira, Ureno
Urefu:
Futi 6 inchi 1 (1.85m)
Uzito:
Kilo 75
MSIMU
ULIOPITA
MECHI
WALIZOCHEZA
Ronaldo
30
Bale 34
MAGOLI
Ronaldo
34
Bale 21
MASHUTI
GOLINI
Ronaldo
235
Bale 165
MASHUTI
YALIYOLENGA
Ronaldo
105
Bale 73
PASI
ZA MABAO
Ronaldo
10
Bale 4
RAFU
WALIZOCHEZA
Ronaldo 27
Bale 24
RAFU
WALIZOCHEZEWA
Ronaldo 81
Bale 47
KADI
ZA NJANO
Ronaldo 9
Bale 6
KADI
NYEKUNDU
Ronaldo 0
Bale 0
******
THAMANI
ZAO
Bale
Bale
alihamia Spurs kutoka Southampton mwaka 2007 kwa kitita cha Pauni milioni 5 tu,
inasemekana anatua Madrid kwa Pauni milioni 78.
Ronaldo
Alitua
Manchester United akitokea Sporting Lisbon ya Ureno kwa kitita cha Pauni
milioni 12.5 mwaka 2003 na kisha akatua Madrid kwa Pauni milioni 80.
(Hii
inamaanisha kuwa ungeweza kuwanunua akina Bale 16 kwa bei ya Ronaldo wakati
ule)
Bale
Kwa
kutazama nje, nyota huyo wa Tottenham Hotspur, anaonekana kwamba ataweza kufiti
katika mfumo wa Real Madrid kama atakuwa mchezaji wa klabu hiyo.
Winga
huyo wa Wales, aina ya soka lake linafanana na la Ronaldo kwa kiasi fulani, kwa
maana ya kasi, nguvu na chenga za aina yake.
Alichukuliwa
na Spurs kutoka katika klabu ya Southampton kwa kitita cha Pauni milioni 5 tu
mwaka 2007. Kipindi hicho, mchezaji huyo ndani ya kikosi cha Spurs ameweza
kupandisha kiwango chake cha soka na kuwa moja ya mastaa wanaotetemesha soko la
usajili kwa kipindi hiki.
Kwa
aina ya uchezaji wake wa sasa, akiwa chini ya kocha Andre Villas-Boas, Bale ameweza
kuonyesha kwamba ni tishio kubwa anapocheza kama mshambuliaji wa kati.
Uwepo
wake kwenye kikosi cha Spurs, ambacho safu yake ya ushambuliaji imekuwa
ikibadilika, lakini kuwapo kwa mchezaji huyo kumeifanya timu hiyo ya Ligi Kuu
England kuwa na makali ya aina yake.
Kama
ilivyo kwa Ronaldo, Bale ni mchezaji wa muda mrefu, kwamba unaweza kuwekeza
kupitia yeye na ukawa kwenye mipango kwa muda mrefu zaidi.
Uwezo
wake wa umaliziaji ni wa aina yake na kuhesabiwa kuwa mmoja wa washambuliaji
ulimwenguni, huku anamiliki pia kiwango kikubwa cha uchezeshaji, kitu ambacho
kinaweza kumpa nafasi ya kucheza katika klabu yoyote. Je, atafiti kwenye mfumo
wa Madrid?
Ronaldo
Ni
straika wa aina yake, ambaye ni gumzo ulimwenguni.
Kumekuwa
na imani kwamba Mreno huyo anatumia uvumi uliopo kwamba alitaka kurudi United
ili kuifanya Real Madrid kutoa fedha nyingi kumbakiza, lakini ukweli halisi
mchezaji huyo alifanikiwa kuishawishi Madrid ikamwongezea mkataba mnono.
Ronaldo
si mchezaji tofauti sana na yule aliyehama United mwaka 2009, kwa sasa amezidi
ubora wake zaidi. Kama Bale atapangwa naye, hakuna shaka kwamba ataendelea
kutumika kama winga, ambayo ni nafasi yake ya asili.
Ni
wazi kabisa kocha wa Madrid anaweza kufanya mabadiliko ya namba kwa ajili ya
kukiweka sawa kikosi chake. Ronaldo atapewa nafasi pia ya kuzunguka uwanja
mzima kutafuta mipira. Na kwenye hilo, Madrid haitaweza kutumia mfumo wa
4-2-3-1 kwa sababu jambo hilo litaacha nafasi kwenye kikosi, hasa kwa upande wa
wachezaji wa pembeni.
No comments:
Post a Comment