LONDON, England
DIRISHA la usajili wa ligi mbalimbali ulimwenguni lilifungwa rasmi usiku wa kuamkia jana, baada ya kila timu kuhakikisha inawanasa nyota wanaoifaa.
Hata hivyo mchakato huo wa uliodumu kwa siku 64 ambazo ni sawa na saa 1536 ulikuwa wa aina yake katika Ligi Kuu ya England, ambapo ilishuhudiwa dakika 60 za mwisho wachezaji kama vile Ozil, Fellaini, Coentrao na Lukaku wakitingisha usajili huo bada ya tetesi za musa wa saa 11.
Mtikisiko huo wa kwenye ulimwengu wa dunia ulikuja siku ambayo tayari
mvutano wa muda mrefu kuhusu usajili wa Gareth Bale, Luis Suarez, Wayne Rooney na
Marouane Fellaini ukiwa umekamilika.
Hata hivyo, hadi saa 11:00 usiku kwa saa za Uingereza, kila kocha alikuwa
bado akihaha kukamilisha usajili wake kabla ya dirisha hilo halijafungwa.Katika dakika hizo 60 kuanzia saa 10.30 usiku hadi saa 11.30 ndipo iliposhuhudiwa kila kocha akipita kila kona ili kuhakikisha anainasa saini ya mchezaji aliyekuwa akimtaka.
Ufuatao ni muda ambao kila kocha alifanikiwa kuwa na uhakika na kile
alichokuwa akikifukuzia kwa muda mrefu na hivyo kupumua.
1.Saa 10.30
usiku, muda huu ndiyo Mesut Ozil alisaini
kwenye fomu za kuitumikia Arsenal
Katika muda huo kocha Arsene Wenger ndipo alipoutangazia umma wa mashabiki wa Arsenal kuwa amevunja rekodi ya klabu hiyo kwa kutoa pauni milioni 42.5 kumsainisha nyota huyo wa Real Madrid.
Katika mkataba huo, mchezaji huyo raia wa Ujerumani alisaini mkataba wa miaka minne na timu hiyo ya Gunners, licha ya vinara wengine wa soka nchini Ufaransa, PSG kutua mezani na ofa ya zaidi ya pauni milioni 140,000 kwa wiki ambazo nyota huyo atakuwa akilipwa kwenye klabu hiyo ya Emirates.
1.11.06 usiku, Marouane Fellaini anamwaga wino kwenye mkataba wa Manchester United
Katika muda huo ndipo ndoto za mchezaji Marouane Fellaini kuungana tena na kocha mpya wa Manchester United, David Moyes zilipotimia.
Katika makubaliano hayo, Everton na Man United zilikubaliana kuuziana raia huyo wa Ubelgiji kwa pauni milioni 27.5.
3. Saa 11.18 usiku. Fabio Coentrao naye asaini mkataba na Manchester United.
Inaelezwa kuwa muda huo ndipo nyota huyo aliyekuwa akiwindwa na kocha wa zamani wa timu hiyo, Alex Ferguson usajili wake ulipokamilika baada ya beki huyo wa kushoto wa timu ya Real Madrid, Coentrao alipowasili kwenye uwanja wa Old Trafford kwa mkopo wa muda mrefu.Hata hivyo inaelezwa kuwa hakuna siri kwamba Moyes alikuwa akimtaka beki wa kushoto wa timu ya Everton lakini hakuna shabiki wa Manchester United anaweza kulalamika kuhusu beki huo.
4. Saa 11.30... Romelu Lukaku anasaini Everton.
Akiwa merejea Chelsea akitokea West Brom ambako alikipiga kwa mkopo wa muda mrefu wengi walikuwa wakitarajia angekuwa chagu la kwanza kwenye safu ya ushambuliaji ya Jose Mourinho.
Hata hivyo kadri wiki zilivyokuwa zikienda, ilishuhudiwa Lukaku akitokea benchi mara tatu ambapo kati ya hizo, mojawapo ni mechi ya ufunguzi wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, ambayo alikosa penalti dhidi ya Bayern Munich na kwa sasa amepelekwa kwa mkopo wa muda mrefu kwenye klabu hiyo ya Goodison Park. Hatua hiyo inatafsiriwa kuwa huenda Mourinho amemuona Lukaku hafai kwenye kikosi kinachosaka ushindi na ndiyo maana akaamua kumpeleka huko.
Kwa kuondoka nyota huyo, Chelsea itakuwa imebaki na washambuliaji Fernando Torres na Demba Ba wakiwa chaguo la pili kwa nyota aliyenunuliwa msimu huu Samuel Eto’o.
Usajili zaidi uk.12&13
No comments:
Post a Comment