HALI ya utata imeonekana kugusa hisia za watu wengi kutokana na kifo cha msanii Albert Mangwea, huku ripoti yake ikifanywa siri, kushindwa kuurudisha mwili wa marehemu nchini Tanzania kwa ajili ya mazishi yake.
Marehemu Ngwea, enzi za uhai wake
Kwa siku tatu sasa, mazishi ya Ngwea yamekuwa yakisogezwa mbele kwa madai kuwa ripoti yake haijamilika. Awali, mwili wa Ngwea ulitarajiwa kufika Tanzania Alhamisi, lakini danadana ilianza hadi sasa kutarajiwa kuletwa mwili wake siku ya Jumatatu au Jumanne.
Kama hivyo ndivyo, mwili wa Ngwea una dalili ya kuzikwa Alhamisi, hasa kama utaratibu wa kuagwa katika Viwanja vya Leaders Club utabaki kama ulivyopangwa.
Akizungumza kwa masharti ya kutajwa jina lake, mtu wa karibu ndani ya Kamati ya Mazishi, haelewi kwanini kifo cha Ngwea kinakuwa cha utata, hadi ujio wake Tanzania kushindwa kueleweka.
Ingawa maandalizi kwa kila hatua yamekuwa yakifanyika, lakini Hospitali ya Dk Hellen nchini Afrika Kusini, imekuwa ikishindwa kutoa majibu ya ripoti ya msiba huo.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba, alisema kuwa kamati yao haiwezi kufanya vitu kinyume na ripoti ya hospitali hiyo.
“Na sisi tunasubiria ndugu yetu aletwe ili shughuli za mazishi yake zifanyike kwa Watanzania wote washiriki kwa namna moja ama nyingine, hivyo tunaomba tuwe na subira katika hili,” alisema.
Kuna kila dalili kuwa Ngwea ataletwa Tanzania Jumanne kama sio Jumatatu, hivyo utaratibu wa mazishi yake kuendelea kama ulivyopangwa na Kamati ya Mazishi.
Msiba wa Ngwea umegusa hisia za watu wengi, huku kwa sasa watu wakikutania nyumbani kwa kaka yake, Kenneth Mangwea, ambaye pia ndio mwenyekiti wa Kamati hiyo ya mazishi.
Aidha, wadau mbalimbali wamekuwa wakijitokeza kusaidia kwa namna moja ama nyingine, hasa katika suala la michango
No comments:
Post a Comment