Manuel Pellegrini. |
Pellegrini raia wa Chile mwenye umri wa miaka 59 amekamilisha kazi yake katika klabu ya Malaga katika mchezo ambao walichezea kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Barcelona katika siku ya mwisho ya ligi kuu ya nchini Hispania "Primera Division".
Pellegrini amenukuliwa akisema: 'Tutaona jumatatu na kuendelea juu ya hatma yangu ya baadaye. Kama makubaliano yatafikiwa tutasema wazi kabisa.
'si kwamba nathibitisha kitu, kwasababu sioni kama inafaa kusema katika misingi ya tetesi, Nina makubaliano ya kuanza mazungumzo na Manchester City.
'Tetesi nyingine huwa kweli na nyingine uongo. Nimekuwa nikiangalia Malaga mpaka sasa.'
'Ni ngumu kuondoka Hispania baada ya miaka tisa. Ni nchi ambayo imenifanyia mazuri sana.
'Hatua ambayo ni kubwa katika kazi yangu na sasa naweza kwenda nchi nyingine.'
Mwenyekiti wa City Khaldoon Al Mubarak jana alinukuliwa akisema wanatarajia kumtangaza meneja mpya ndani ya siku kumi.
No comments:
Post a Comment