MANCHESTER,
England
MSHAMBULIAJI
wa Manchester United, Wayne Rooney (27) anajiona kama amewekwa kwenye wakati
mgumu na kusalitiwa, baada ya mazungumzo yake binafsi na Sir Alex Ferguson
kuvuja.
Alipoingia
ofisini kwa Ferguson, wiki tatu zilizopita, Rooney alihitaji majibu ya kwanini
anaonekana kama siyo sehemu muhimu ya Man United.
Kwa mujibu
wa mtu wa karibu na Kambi ya Rooney, anasema Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa
muhimu Old Trafford, tangu alipotua mwaka 2004, alikuwa amepania kumuuliza
Fergie kwa nini anaonekana amepoteza imani naye.
Rooney
alihitaji kujua ana nafasi gani ndani ya kikosi cha Ferguson siku zijazo, na
alimwambia wazi Fergie kuwa hataki kuwa na msimu mwingine mgumu kama huu
akihamishwahamishwa kikosini.
Lakini baada
ya kumaliza kikao chake na Fergie dakika 25 baadaye, Rooney alikuwa hana
uhakika na mustakabali wake Old Trafford, kutokana na Ferguson kutomuahidi
lolote, juu ya nafasi yake kwenye timu.
Cha ajabu
kila kitu kilichotokea kwenye mazungumzo yake na Fergie kilivuja, kitu ambacho
kimemfanya Rooney ajione kama anatafutiwa sababu ya kuondolewa Man United, huku
Red Devils wakipiga hatua ya kwanza katika kile kinachoonekana kama mwisho
wake.
Mtu huyo wa
karibu na Rooney anasema wazi anaamini kuwa, majadiliano yake na Fergie
hayakutakiwa kutangazwa hadharani, japokuwa hataki kuamini kuwa Ferguson ndiye
aliyevujisha siri hiyo.
Rooney
anajiona kama amesalitiwa kutokana na kuvuja kwa habari hizo, huku akishitushwa
na taarifa kwamba aliweka mezani madai ya kuondoka Old Trafford, kitu ambacho
anakikanusha kwa nguvu zote.
Man United,
wamekanusha taarifa kuwa Rooney aliomba kuondoka, tayari klabu hiyo imesema
kwamba, haina mpango wa kumuuza.
Inasemekana
Rooney na Ferguson, walikubaliana kulijadili jambo hilo kwa kina baada ya mechi
dhidi West Brom, Jumapili ijayo. Lakini Sasa hivi Rooney haelewi nini kitamkuta
baada ya Fergie kustaafu.
Sakata hilo
ndio kitu cha kwanza kitakachotua kwenye meza ya David Moyes, Julai 1,
atakapoanza kazi rasmi, labda kama Man United wakiamua kumuuza kabla ya hapo.
Gwiji wa Man
United, Bryan Robson amemshauri David Moyes kumshawishi Rooney kubaki Old
Trafford, kwa sababu kufanya hivyo itakuwa hatua ya kwanza muhimu kwake katika
kujitengenezea jina miongoni mwa mashabiki wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment