Nicola Rizzoli |
Mwamuzi kutoka Italia Nicola Rizzoli ametangazwa kuchezesha mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baina ya Borussia Dortmund dhidi ya Bayern Munich mchezo utakao pigwa katika uwanja Wembley siku ya jumamosi.
Mwamuzi huyo mwenye miaka
41- amekuwa mwamuzi wa kimataifa tangu mwaka 2007.
alichezesha mechi ya kwanza ya
fainali ya ligi ya Ulaya mwaka 2010 iliyochezwa uwanja wa
Hamburg, ambapo Atlético de
Madrid iliifunga Fulham FC 2-1 katika muda wa nyongeza, na
amechezesha mechi tatu katika michuano ya ulaya EURO 2012.
Kiujumla , Rizzoli amechezesha na
kuhusika katika mechi 26 za ligi ya mabingwa barani ulaya ,nne kati ya
mechi hizo ni za msimu huu ikiwemo ya mkondo wa pili wa hatua
ya 16 kati ya Málaga CF na FC Porto.
Mwamuzi huyo atasaidiwa
na Waitaliano wenzake Renato Faverani na Andrea
Stefani na mwamuzi wa mezani atakuwa Damir
Skomina kutoka Slovenia.
Waamuzi wengine wa
akiba ni Gianluca Rocchi na Paolo Tagliavento wote
kutoka Italia waamuzi ambao watakuwa katika benchi kama mabao yataharibika
ni Gianluca Cariolato ambao wanamaliza timu ya waamuzi wa mchezo huo
.
.
No comments:
Post a Comment