Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 25, 2013

WANYAMA ANG'ARA CELTIC, AMSHUKURU NEIL LENNON

Victor Wanyama


GLASGOW, Scotland
KIUNGO wa kimataifa wa Kenya, anayekipiga katika klabu ya soka ya Celtics FC, Scotland, Victor Wanyama, amejivunia mafanikio ya timu yake ambayo imetwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo katika Ligi Kuu ya soka nchini humo.

Wanyama ambaye amekuwa na Celtics tangu Julai 2011, amesema amekuwa na misimu miwili yenye mafanikio kwa klabu hiyo na anaamini ametoa mchango muhimu kwa timu hiyo kutwaa ubingwa msimu huu. “Nilipojiunga na timu hii sikuwa nafahamika, na zaidi nchi yangu haikuwa moja kati ya nchi zenye majina makubwa kwenye soka, taratibu uwezo wangu ulikuwa ukipanda na kupata namba kwenye timu, nikiwa hapa tumetwaa mataji mawili na nimekuwa na namba kwenye kikosi na nafurahi kwamba nimekuwa nikiaminiwa katika mechi ngumu ambazo tumecheza na kushinda kama ile ya Barcelona,” alisema Wanyama.

Wanyama pia alimshukuru kocha wake, Neil Lennon kutokana na kuonyesha imani kwake na kumsaidia kwa kiasi kikubwa kujenga kipaji chake katika soka la Kimataifa.
“Amekuwa si kocha tu, bali ni rafiki, amenifanya nijiamini uwanjani na kuona kuwa yote yanawezekana, namshukuru sana na sasa nimo kwenye kikosi cha mabingwa mara mbili, hili ni suala kubwa kwangu na kwa Wakenya wote,” alisema.
Nyota huyo wa Kenya, alijiunga na Celtic akitokea klabu ya  Germinal Beerschot ya nchini Ubelgiji. 

No comments:

Post a Comment