Kocha Kim Poulsen na Erasto Nyoni wakishuka baada ya kuliona basi lilivyo huko ndani
Rais wa TFF, Leodgar Tenga akisaini mpira
Basi lililotolewa na (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro
Mdau akiwa amejichora rangi za bendera ya Taifa
Kocha Kim akisaini mpira
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Robin Goetzsche (wa pili kushoto) akikabidhi funguo kama ishara ya kukabidhi basi la Taifa Stars kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Leodgar Tenga (wa tatu kushoto) wakati Kilimanjaro Premium Lager ilipokabidhii basi hilo leo makao makuu ya TBL Jijini Dar es Salaam. |
Kocha Kim Poulsen na Erasto Nyoni wakishuka baada ya kuliona basi lilivyo huko ndani
Rais wa TFF, Leodgar Tenga akisaini mpira
Basi lililotolewa na (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro
Mdau akiwa amejichora rangi za bendera ya Taifa
Kocha Kim akisaini mpira
Wakaguzi wa ukanda wa Afrika wa brand ya bia ya Kilimanjaro
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya
Kilimanjaro ambao ni wadhamini wa timu ya taifa ya (Taifa Stars) leo
wamekabidhi rasmi basi la timu hiyo yenye dhamani ya zaidi ya million 200.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa bia ya
Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa basi hilo lina uwezo wa kubeba abiria
51, uwezo wa injini ni 300 HP Cummins na kumeza lita 800 za mafuta.
Kavishe alifafanua kuwa TBL limenunua basi hilo ikiwa ni
sehemu ya ufadhili kama ilivyoaishwa katika mkataba baina ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) na kampuni hiyo.
“Imeshatimia miezi 10 tangu toka TBL ilipoanza kufadhili
Taifa Stars na malengo yetukama wadhamini ni kuiona timu ikipata ushindi
uwanjani na kuongeza sifa ya timu na tumerithika na matoke,”Alisema.
Alisema kuwa TBL itaendelea kusaidia timu ya taifa na hivyo
kupandisha kiwango cha soka nchini ili baadae waweza kupata nafasi ya kushiriki
michuano ya Afrika na baadae kombe la dunia.
Nae Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Leodegar
Chilla Tenga alihaidi kulitunza basi hilo kwa mafanikio ya timu hiyo ya Taifa
ambayo kwa sasa inafanya vema katika michezo mbalimbali.
Tenga alisema kuwa ujio wa basi hilo ni ishara
nzuri ya kuifikisha timu hiyo kwenye mafanikio zaidi
No comments:
Post a Comment