JAMALI MALINZI
SLP 10000 DAR ES SALAAM
13/FEBRUARI/201
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
YAH:KUENGULIWA KWANGU KUGOMBEA URAIS WA TFF
2013
Ndugu zangu, kupitia vyombo vyenu vya habari ninaomba
nieleze umma wa watanzania hususani wadau wa mpira wa miguu yafuatayo kuhusu
kuenguliwa kwangu.
Awali ya yote nieleze kusikitishwa kwangu na maamuzi
yaliyotolewa na kamati ya rufaa ya TFF ya kuniengua kugombea urai s wa
TFF.Sikubaliani na maamuzi yaha.
Katika kuniengua kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF
imetoa sababu mbili (nanukuu magazeti ya jana tarehe 12/02/2013 maana hadi leo
sijakabidhiwa barua ya kuenguliwa)
1.Kukosa uadilifu kwa kupinga waraka uliotolewa na TFF
wa kubadili katiba ya TFF mwezi Desemba 2012.
2.Kukosa uzoefu wa miaka mitano ya
uongozi.
Ndugu zangu kiini cha maamuzi ya kamati ya rufaa dhidi
yangu ni pingamizi lililowekwa na mtu mmoja anayeitwa AGAPE FUE. Bwana Agape Fue
aliniwekea pingamizi katika kamati ya uchaguzi akidai mimi nilipinga waraka wa
kubadili katiba ya TFF na pia sina uzoefu uzoefu wa mika mitano ya uongozi wa
mpira. Kinyume na matakwa ya kamati ya uchaguzi kama yalivyotangazwa kuwa mtoa
pingamizi aje mwenyewe kutetea pingamizi lake , bwana Agape Fue hakutokea mbele
ya kamati ya bwana Lyato. Matokeo yake tarehe 31/01/2012 kamati ya uchaguzi ya
TFF ilitoa maamuzi ya kutupilia mbali pingamizi
hilo.
Bwana Agape Fue hakuishia hapo kwa mara nyingine tarehe
06/02/2013 alikata rufaa kwenye kamati ya rufaa ya uchaguzi akidai kamati ya
uchaguzi haikumtendea haki. Rufaa hii haikuwa na anwani wala namba ya simu ya Bw
Agape Fue ilisikilizwa tarehe 10/02/2013 na maamuzi ya kukata jina langu
yakatangazwa jioni ya tarehe 11/02/2013.
Mpaka leo najiuliza hivi huyu Bw Agape Fue ni mwanaume
au ni mwanamke? (hakueleza kama ni Bwana au Bibi Agape Fue). Agape Fue ni nani
hasa? Anaishi wapi? Je ni Mtanzania au sio Mtanzania maana kikanuni wasio
watanzania hawaruhusiwi kujihusisha na uchaguzi wa TFF (rejea kifungu cha 9 cha
kanuni za uchaguzi),pingamizi lake halikuambatana na udhibititisho wa uraia. Kwa
nini alichukua maamuzi haya? Sipata jibu. Iweje achukue maamuzi mazito ya
kumkatia mtu rufaa kisha uishie kusaini karatasi na kwaachia wengine wakusemee
na usije hata kushuhudia kinachoendelea kama kweli una maslahi na madai yako?
Waandishi wa habari mnisaidie kupata majibu.
Ndugu zangu, mtoa pingamizi alidai haikuwa sahihi
kupinga azimiao la kubadili katiba ya TFF kwa njia ya waraja . Naomba nisisitize
mambo matatu:
1.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF wanawakilisha matakwa ya
vyama vilivyowatuma kwenda kwenye mkutano mkuu wa TFF, na ndio ndio maana chama
cha mpira cha mkoa wa Kagera(KRFA) kiliitisha kikao cha kamati ya utendaji ili
kamati iweze kutoa mwongozo kwa wajumbe wake kuhusu nini kifanyike kuhusu waraka
ulioletwa na TFF, hivyo maamuzi ya yaliyotolewa ya kuukataa waraka huo yalikuwa
ni maamuzi ya chama cha mpira mkoa wa Kagerana wala haya kuwa maamuzi maamuzi ya
Jamali Malinzi, iweje Malinzi niadhibiwe kwa maamuzi haya, kwani nini
usiadhibiwe mkoa mzima na mikoa yote iliyopinga waraka? Hii ni haki kweli?
Siamini kama kuna mjumbe wa mkutano mkuu aliyekiuka maamuzi ya kamati yake ya
utendaji.
2.
Katika mchakato wa kubadili katiba kwa njia ya waraka
kilichokuwa kinagomba sio maudhui (content) ya mabadiliko ya katiba bali
utaratibu uliotumika kubadili katiba. Swali la msingi tulilojiuliza ni wajumbe
wa kamati ya utendaji KRFA ni kwamba je kwa mujiibu wa katiba ya TFF kifungu 22
na kifungu 30 wapi katiba inatamka kuwa inaweza kubadilishwa kwa njia ya waraka?
Mpaka leo hilo jibu hakuna , labda aliyeniwekea pingamizi atusaidie kupata jibu
la swali hili. Katiba ya TFF iko wazi kabisa inatamka kuwa katiba itabadilishwa
kwa njia ya mkutano mkuu tu( General assembly).
3.
Ni kweli FIFA iliagiza yafanyike
mabadiliko ya katiba ya kuingiza kipengele cha ‘club licencing’ katika katiba ,
lakini je FIFA katika agizo hilo ilisema katiba ya ya TFF ivunjwe ili kutimiza
azma hiyo? Ikimbukwe kuwa mwaka 2004 FIFA iliagiza TFF aiingize kwenye katiba
kipengele cha katibu mkuu awe wa kuajriwa badala ya kuchaguliwa, agizo
lilitekelezwa kwa kupitishwa na mkutano mkuu wa TFF, iweje leo utaratibu huu
ukiukwe? Hata majuzi CAF walipotaka kubadili katiba ili Rais wa CAF atokane na
wajumbe wa kamati ya utendaji jambo hili lilitekelezwa kwa kuitisha mkutano mkuu
wa dharura uliofanyika Seychelles majuzi. Katiba ndio msingi mkuu
wa uendeshaji wa TFF, nitaipigania siku zote. Huu ndio utaratibu ,
si CAF si FIFA si vyama vyama vya mpira vya nchi, hakuna
anayebadili katiba kwa njia ya waraka, kama kuna mwenye ushahidi
aulete.
Kuenguliwa jina langu eti kwa kuwa nilipinga waraka wa
kubadili katiba sio uamuzi sahihi.
Kuhusu uzoefu wa miaka mitano katika
uongozi:
Ikumbukwe kuwa katika uchaguzi wa TFF mwaka 2008
niligombea na jina langu lilikatwa na kamati ya uchaguzi ya TFF.
Nilikata rufaa katika kamati ya rufaa ya TFF na kushinda . Hukumu hii ni
halali hadi leo . Iweje leo miaka minne baadaye kamati hiyo hiyo ya rufaa (
kubadili kubadili majina ya wajumbe sio kubadili taasisi) inione sina uzoefu? Si
hilo tu, hata katika kujaza fomu namba moja ya kugombea niliambatanisha
vielelezo vyote vya uzoefu wangu ikiwa ni pamoja na kudhibitisha kuwa katika
kipindi cha miaka minne iliyopita nimekuwa :
-Mjumbe wa Baraza la michezo mkoa wa Dar es
Salaam.
-Mwenyekiti wa kamati ya mashindano chama cha mpira
mkoa wa Pwani COREFA.
-Mjumbe wa mkutano mkuu wa mkoa wa
Kagera.
-Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa
Kagera.
Hii ni pamoja na kuongoza Yanga 2002
-2005
Hivi katika nafasi hizi za uongozi ipi ni ya kuongoza
‘Bonanza’? Nimedhalilishwa sana.
HITIMISHO.
Vyombo vya habari kupitia nakala, tahariri na maoni ya
wasikilizaji /wasomaji/watazamaji vimesifia sana awamu mbili za uongozi wa Bwana
Tenga. Bwana Tenga amesifiwa kwa umahiri wake wa kuleta utulivu katika sekta ya
mpira wa miguu Tanzania. Amesifiwa kwa kujenga taasisi imara ambayo mhimili wake
mkuu ni sekretarieti makini na kamati mbaloimbali zilizo imara. Let him rise to
the occasion, muda wa kuonyesha uongozi imara ni huu, historia itamhukumu kwa
jinsi gani atasimamia suala hili , haki sio lazima itendekea lakini pia
inatakiwa ionekane inatendekea.
Kamati ya utendaji ya TFF inayo mamlaka ya kubatilisha
maamuzi haya kwa maslahi ya mpira wa Tanzania. Ninamshauri Rais wa TFF aitishe
kikao cha dharura cha kamati ya utendaji ili kijadili hali hii na kunirudishia
haki yangu ya kugombea urais wa TFF.
Nihitimishe kwa kuwaomba wadau wa mpira wa miguu
Tanzania wawe watulivu wakati tukisubiri kupata ufumbuzi wa suala
hili
Mungu ibariki Afrika,
Mungu ibariki Tanzania.
Ahsanteni sana.
Jamali Emil Malinzi
Dar es Salaam
13/02/2013
No comments:
Post a Comment