Juma Nassoro amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha waamuzi Taifa (FRAT) baada ya kupata kura 15 kwenye uchaguzi uliofanyika leo mjini Mororgoro
Uchaguzi huo ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa Savoi ulishuhudia Said Nassoro akimbwaga Army Sentimea aliyepata kura 4 na kura tisa zikiharibika.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilichukuliwa na Juma Chaponda aliyepata kura 27, baada ya kuwazidi Juma Mpuya aliyepata kura nne na Tifika Kambimtoni kura sita
Nafasi ya Katibu Mkuu imechukuliwa na Charles Ndagala kura 27, aliwaacha mbali mpinzani wake Abdallah Mitole aliyepata kura saba, na Hamis Kisiwa akiambulia kura mbili.
Nafasi ya Mhazini ambayo ilikuwa na mgombea mmoja, Jovin Ndimbo amepata kura 27 moja ikiharibika.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Kamwaga Tambwe aliyepata kura 18 na kura saba zikimkataa wakati nafasi ya uwakilishi wanawake imechukuliwa na Isabela Kapera aliyepata kura 27 huku moja ikimkataa
Akizungumza kwa njia ya simu Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Damas Ndumbaro alisema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kila mmgombea wamekubaliana na matokeo.
“Uchaguzi ulikuwa huru na hakuna malalamiko yeyote kamati iliyopokea hadi muda huu”, alisema Ndumbaro.
Uchaguzi huu unafanyika baada ya kuharishwa mara kadhaa kwa kukiuka kanuni za uchaguzi za shirikikisho la soka nchini sababu iliyopelekea aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo Alhaj Muhidin Ndolanga kuondolewa kuiongoza kamati hiyo.
No comments:
Post a Comment