SHIRIKISHO la Ngumi la
Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati limewaalika
wafanyabishara wa Tanzania kuhudhuria mkutano wa mwaka wa IBF/USBA
utakaofanyika katika jiji la Berlin nchini Ujerumani kuanzia Mei 21-25 mwaka
huu.
Katika mkutano huo
wanachama zaidi ya 3000 wa IBF/USBA kutoka nchi zaidi ya 200 duniani
watahudhuria.
Taarifa iliyotumwa na
Rais wa IBF Bara la Afrika na Ghuba ya Uajemi, Onesmo Ngowi, ilisema hiyo ni fursa
pekee kwa wafanyabishara wa Kitanzania kuweza kutumia mkutano huo kutangaza
biashara zao katika sekta mbalimbali hususan sekta ya Kitalii, TEHAMA,
usafirishaji wa bidhaa za Tanzania nje ya nchi pamoja na uwekezaji katika sekta
mbalimbali nchini.
Mkutano wa mwaka wa
IBF/USBA huwakutanisha wafanyabishara waliowekeza katika sekta mbalimbaki za
kiuchumi na hutoa fursa kubwa kwa wafanyabishara kujenga mitandao mzuri wa
biashara.
Aidha, Ngowi
anawahamasisha wakuzaji wa mchezo wa ngumi pamoja na wale wanaofanya shughuli
za Branding (kukuza biashara) kuhudhuria mkutano huu na kujipatia fursa
mbalimbali za biashara.
Ngowi ataongoza ujumbe
nzito kutoka bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati wakiwamo
Mawaziri wa Michezo kadhaa kutoka nchi zilizo katika ukanda huu.
No comments:
Post a Comment