Wakati mchakato wa uchaguzi ndani ya shirikisho la
soka nchini TFF na bodi ya ligi kuu ukizidi kupamba moto huku baadhi ya wagombea
wakiwekewa mapingamiz na wadau mbalimbali wa soka nchi hatimaye pingamizi
alilowekewa mgombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti Said Mohamed
limeondolewa.
Pingamizi liliwekwa kwa mgombea huyo lilitoka kwa
katibu wa zamani wa chama cha soka mkoa wa kisoka wa Kinondoni Frank Mchaki
ambaye aliweka pingamizi hilo kutokana na kwamba mgombea huyo hakuwa kiongozi wa
klabu yoyote nchini.
Hata hivyo kufuatia kamati ya uchaguzi kukutana na
wagombea na wawekaji wa mapingamizi hayo kwa lengo la kufanyika mapitio ya
mapingamizi mbalimbali na sababu za mapingamizi hayo imedhihika kuwa Mzee Said
Mohamed ni kiongozi wa Azam fc kwa nafasi ya
mwenyekiti.
Akiongea na waandhishi wa habari hii mwekaji wa
pingamizi hilo Mchaki amesema ameridhishwa na zoezi la kuhakiki nafasi ya
uongozi ya mzee Said Mohamed ndani ya Azam kwani aliweka pingamizi kwa kuwa
alikuwa hana uhakika kama Said Mohamed ni kiongozi wa kuchaguliwa wa Azam licha
ya kwamba amekuwa akisikia kuwa ni kiongozi wa klabu
hiyo.
Mchaki amesema mzee Said Mohamed alikuja na
vielelezo kamili ambavyo vimeonyesha kuwa alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti
1/10/2012 alikuwa ni mwenyekiti wa Azam.
Kumbuka moja ya sifa ya kuwania nafasi ya uongozi
ndani ya bodi ya ligi, mgombea anapaswa kuwa kiongozi katika moja ya vilabu vya
ligi kuu.
No comments:
Post a Comment